Pata taarifa kuu
SYRIA-SIASA

Syria yafanya uchaguzi wa urais

Vituo vya kupigia kura vmefunguliwa kote Syria leo Jumatano kwa uchaguzi wa urais ambapo rais  unaotarajiwa kumpa ushindi Bashar al Assad kwa muhula wa nne wa miaka saba

Asma, mke wa Rais wa Syria Bashar al-Assad, anapiga kura wakati wa uchaguzi wa urais huko Douma, Syria, Mei 26, 2021.
Asma, mke wa Rais wa Syria Bashar al-Assad, anapiga kura wakati wa uchaguzi wa urais huko Douma, Syria, Mei 26, 2021. VIA REUTERS - SANA
Matangazo ya kibiashara

Serikali inasema uchaguzi unaonyesha kuwa Syria inafanya kazi kawaida, licha ya vita vya miaka kumi. Lakini wapinzani na nchi za Magharibi wanaona zoezi hilo kama kichekesho kilichokusudiwa uweka kando ushawishi wa Bashar al-Assad katika utawala.

Zaidi ya watu milioni 18 wana haki ya kupiga kura ndani na nje ya Syria kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mohammed al Rahmoun.

Kwa msaada wa Iran na Urusi, al-Assad ameweza kuchukua tena udhibiti wa zaidi ya asilimia 60 ya nchi. Waasi bado wanashikilia maeneo kadhaa kaskazini na kaskazini magharibi mwa Syria, wakati Wakurdi wanatawala maeneo ya kaskazini mashariki.

Al-Assad, mwenye umri wa miaka 55 anatarajiwa kushinda muhula wa nne wa miaka saba katika uchaguzi wa leo ambao upinzani umeutaja kuwa ni wa undanganyifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.