Pata taarifa kuu
SYRIA

Bashar al Assad kuwania kiti cha urais kwa muhula wa 4 Mei 26

Rais wa Syria Bashar al Assad Jumatano wiki hii amewasilisha nyaraka za kuwania muhula wa nne katika uchaguzi wa urais wa Mei 26, spika wa Bunge la Syria ametangaza kwa vyombo vya habari vya serikali.

Rais wa Syria Bashar al-Assad wakati wa mahojiano huko Damascus, Machi 5, 2020.
Rais wa Syria Bashar al-Assad wakati wa mahojiano huko Damascus, Machi 5, 2020. AFP Photos/SANA
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili Bunge la Syria lilitangaza kwamba uchaguzi ujao wa urais utafanyika Mei 26, uchaguzi ambao Washington na upinzani wa Syria waliutaja kama udanganyifu unaokusudia kuanzisha utawala wa kimabavu.

Kulingana na sheria za uchaguzi, wagombea wanaotaka kuwania katika kinyang'anyiro hiki wanatakiwa wawe waliishi nchini Syria kwa miaka kumi kabla ya uchaguzi huo, hali ambayo inazuia wagombea wakuu wa upinzani wanaoishi uhamishoni.

Familia ya Rais Assad na Chama chake cha Baath wametawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miongo mitano wakisaidiwa na idara za usalama zenye nguvu na jeshi viliopewa uwezo mkubwa wa kifedha na vifaa.

Uchaguzi huu mpya unafanyika miaka kumi baada ya ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya maandamano ya kidemokrasia ambayo yaliiingiza Syria katika vita vikali.

Ukiungwa mkono na Moscow na Tehran, utawala wa Bashar al-Assad sasa umepata udhibiti wa maeneo mengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.