Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Syria: Watu 27 wauawa katika shambulio Damescus na mashambulizi ya anga Idlib

Watu wasiopungua 27 waliuawa siku ya Jumatano katika shambulio dhidi ya basi la jeshi huko Damascus, na kufuatiwa na shambulizi la angala vikosi vya serikali katika maeneo ya waasi kaskazini magharibi mwa nchi. Machafuko yameongezeka nchini Syria kwa miezi kadhaa.

Shambulio hilo, ambalo ni baya zaidi katika mji mkuu wa Syria tangu miaka minne iliyopita, bado halijadaiwa na kundi lolote.
Shambulio hilo, ambalo ni baya zaidi katika mji mkuu wa Syria tangu miaka minne iliyopita, bado halijadaiwa na kundi lolote. AFP - DELIL SOULEIMAN
Matangazo ya kibiashara

Mabomu mawili yaliyotegwa ndani ya basi la jeshi yalilipuka mapema asubuhi wakati ilipopita karibu na daraja katikati mwa mji wa Damascus na kuua watu 14 na kujeruhi angalau wengine watatu, shirika la habari la serikali la SANA limesema.

Kulingana na shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), ambacho kina mtandao mkubwa wa vyanzo nchini Syria, wote waliouawa ni wanajeshi.

Shambulio hilo, ambalo ni baya zaidi katika mji mkuu wa Syria tangu miaka minne iliyopita, bado halijadaiwa na kundi lolote. Lakini vikosi vya serikali vimetekeleza shambulizi la angani katika mkoa wa Idlib, ngome kuu ya mwisho ya wanajihadi na waasi kaskazini magharibi, saa moja baadaye, na kuua watu kumi na tatu, wengi wao wakiwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.