Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Washington yamteua Rina Amiri mjumbe wa haki za wanawake Afghanistan

Miezi sita baada ya kujiondoa kutoka Afghanistan, Jumatano, Desemba 29, Marekani ilimteua mjumbe wa kutetea haki za wanawake katika Imarati ya Kiislamu ya Taliban (Afghanistan). Rina Amiri, 53, aliyezaliwa nchini Afghanistan, atahusika na "maswala muhimu" kwa utawala wa Biden.

Marekani ilitangaza siku ya Jumatano kumteua Rina Amiri, mjumbe maalum wa wanawake nchini Afghanistan. Hapa ilikuwa Septemba 25, 2021, wakati wa kikao kilichoitwa "Rise For And With The Women Of Afghanistan: Los Angeles" huko West Hollywood, California.
Marekani ilitangaza siku ya Jumatano kumteua Rina Amiri, mjumbe maalum wa wanawake nchini Afghanistan. Hapa ilikuwa Septemba 25, 2021, wakati wa kikao kilichoitwa "Rise For And With The Women Of Afghanistan: Los Angeles" huko West Hollywood, California. Randy Shropshire GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Hali mbaya ya wanawake wa Afghanistan imekuwa kipaumbele cha utawala wa Biden tangu kurudi madarakani kwa Taliban. Kipaumbele ambacho kitasimamiwa na Rina Amiri. Waaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani hana majukumu kwake baada ya ukosoaji wake mkali wakati wa kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan. Aliita mchakato wa kuwahamisha wanawake waliokuwa katika hatari wakati huo "janga."

Jumatano hii, Antony Blinken alimteua kuwa mjumbe maalum wa Joe Biden kwa haki za wanawake na wasichana nchini Afghanistan. "Faili zenye umuhimu mkubwa kwangu," anahakikishia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, ambaye anachukua fursa hiyo kusisitiza nia yake ya kuwa na Afghanistan "jumuishi" chini ya utawala wa Imarati ya Kiislamu ya Taliban (Taliban).

Utawala wa zamani wa Obama

Akiwa na umri wa miaka 53, Rina Amiri si mgeni. Mmarekani huyo aliyezaliwa Afghanistan, alikuwa mshauri katika Umoja wa Mataifa na serikali kwa karibu miaka ishirini. Yeye ni afisa wa zamani wa utawala wa Obama.

Katika Gazeti lililochapishwa mwezi Novemba kwenye tovuti ya Sera ya Kigeni, Rina Amiri alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzindua upya mazungumzo ya kidiplomasia na Taliban, bila kutambua utawala wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.