Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Wataliban waitimua jamii ya Hazara kwa nguvu kutoka ardhi zao

Wakati Afghanistan inakabiliwa na ukame, mgogoro wa kiuchumi na mizozo inayozidi kuongezeka, maafisa wa Taliban wamewafukuza maelfu ya wakaazi, hasa kutoka jamii ya Washia ya Hazara, kutoka ardhi zao ili kuwagawanya tena kwa wafuasi wao, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema.

Mtu kutoka jamii ya Hazara akiwa shambani mwake huko Bamiyan, katikati mwa Afghanistan, Oktoba 2, 2021.
Mtu kutoka jamii ya Hazara akiwa shambani mwake huko Bamiyan, katikati mwa Afghanistan, Oktoba 2, 2021. BULENT KILIC AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu Taliban iingie madarakani mwezi Agosti, mamia ya familia za Hazara wamefukuzwa kutoka ardhi zao. Maafisa wa Taliban wanawaamuru "waondoke majumbani mwao na mashambani, huku wakipewa siku chache tu na bila hatua yoyote ya kisheria kuthibitisha haki zao za kumiliki ardhi" Human Rights Watch limesema katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Oktoba 22.

Jamii ya wachache wanyanyaswa

Hatua hii ya kufukuzwa ambayo, kulingana na HRW, ni sawa na "adhabu ya pamoja". Watukutokajamii hii ya Washia kwa muda mrefu wamekuwa wakiteswa na Taliban. Walipoingia madarakani kwa mara ya kwanza, kati ya mwaka 1996 na 2001, walikuwa waathiriwa wa mauaji ya umati yalityotekelezwa na kundi hili la Kiislamu. Kwa upande wa Human Rights Watch, wanasema kufukuzwa huko, ni njia ya kuwatesa zaidi.

"Wataliban hutumia kisingizio cha mizozo ya eneo kuwafukuza watu hawa na wanafanya hivyo kwa kupendelea wafuasi wao, wale ambao wako upande wao katika vita," amebaini  Patricia Gossman, naibu mkurugenzi wa Human Rights Watch katika ukanda wa Asia. Katika majimbo mengine, watu kutoka jamii ya Hazara hufukuzwa kutoka makwao. Ni jmii ya wachache ambayo kwa muda mrefu imepata unyanyasaji kutoka kwa Taliban. Kwa hivyo ni njia ya Taliban kuwalipa wafuasi wao wakati wanapoadhibu wale wanaowachukulia kama maadui zao, hasa jamii ya Hazara. Wanasema kwamba ardhi hizi hazikuwa mali yao kwa kuwa serikali iliyopita ilikuwa ya kifisadi na kwa hivyo maamuzi ambayo huenda yalichukuliwa wakati huo hayana nafasi tena. "

Mikoa mitano inahusika: mwanzoni mwa mwezi Oktoba, Helmand, iliyoko kusini mwa Afghanistan, na Balkh, kaskazini, na kabla ya hapo, Daikundi, Uruzgan na Kandahar.

Kulingana na HRW, watu wanaohusishwa na serikali iliyopita pia wanakabiliwa na hatua hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.