Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Ujerumani yaahidi euro Milioni 50 kwa kuisaidia Afghanistan

Umoja wa Mataifa unasema umeunda mfuko maalum, kukusanya fedha zitakazowasaidia wananchi wa Afganistan.

Mjumbe wa Urusi kwa Afghanistan Zamir Kabulov akisalimiana na Mawlawi Shahabuddin Dilawar, mwakilishi wa ujumbe wa Taliban ambaye alikuja Moscow kwa mazungumzo, Oktoba 21, 2021.
Mjumbe wa Urusi kwa Afghanistan Zamir Kabulov akisalimiana na Mawlawi Shahabuddin Dilawar, mwakilishi wa ujumbe wa Taliban ambaye alikuja Moscow kwa mazungumzo, Oktoba 21, 2021. Via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Ujerumani imekuwa nchi ya kwanza, kuahidi Euro Milioni 50 kwa ajili ya wananchi wa Afganistan wakati huu Umoja wa Mataifa ukiomba wahisani wengine kujitokeza.

Siku ya Jumatano, Urusi iliandaa mkutano kuhusu namna ya kuisaidia Afghanistan na kusema kundi la Taliban linajaribu kuhakikisha kuwa nchi inakuwa thabiti, lakini inarudishwa nyuma na makundi ya kigaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ameonyesha jinsi gani hali ya usalama inavyoyumbishwa, na makundi yanayohusishwa katika kujaribu kuhatarisha usalama wa nchi.

Hali inayoendelea kushuhidiwa nchini Afghanistan haiwezi kuelezwa kuwa thabiti. Kuna makundi mbalimbali ya kigaiadi yanayojaribu kuchukua maeneo ya nchini hiyo, kama Islamic State na al-Qaeda, ambayo yanajaribu kuinua vichwa vyao na kujaribu kutekeleza mashambulizi kila kona ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.