Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Nchi za Magharibi zaamua kuendelea kuondoa raia wao Afghanistan

Milipuko miwili ambayo imesababisha vifo vya watu wengi karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, nchini Afghanistan Alhamisi hii Agosti 26 imezua hofu na wasiwasi mkubwa mongoni mwa raia.

anajeshi wa Taliban mbele ya uwanja wa ndege wa Kabul baada ya milipukomiwili iliyoua watu kadhaa Alhamisi, Agosti 26.
anajeshi wa Taliban mbele ya uwanja wa ndege wa Kabul baada ya milipukomiwili iliyoua watu kadhaa Alhamisi, Agosti 26. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Magharibi zimeapa kuendelea na zoezi la kuwaondoa raia wao hadi agosti 31 licha ya mashambulio hayo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amelaani vikali mashambulio ya "yanayohuzunisha" yaliyotokea katika uwanja wa ndege wa Kabul, ambao uliua watu wasiopungua sita, na kujeruhi makumi ya wengine. "Matukio ya alasiri hii yanaonyesha kuwa hatari ni kubwa na kwamba ni hali ya wasiwasi sana kwa kuwaondoa kutoka nchini humo," Kansela ameongezea katika mkutano na waandishi wa habari. "Tunajua dirisha la kalenda linafungwa na makumi ya maelfu ya watu wamewekwa katika eneo salama, lakini nataka nithibitishe leo kwamba tusisahau kuchukuwa utaratibu mwingine", ameonza Angela Merkel.

►Soma pia: Afghanistan: milipuko mibaya yatokea karibu na uwanja wa ndege wa Kabul

Katika muktadha huu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, Jens Stoltenberg amebaini kwamba kipaumbele "kinabaki kuhamisha watu wengi iwezekanavyo". Hoja iliyoungwa mkono na Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye amesema kuwa operesheni za uokoaji kutoka Afghanistan zitaendelea licha ya mashambulio "ya kinyama" mbele ya uwanja wa ndege wa Kabul, ambayo yamesababisha vifo vya watu sita na wengine kadhaa wakijeruhiwa, amesema Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.

Baada ya shambulio hili, Ufaransa imetangaza kumrejesha Paris balozi wake nchini Afghanistan, David Martinon, kwa sababu za usalama, wakati alikuwa katika uwanja wa ndege wa Kabul kusimamia zoezi la kuwaondoa raia wa nchi hiyo. Baada ya milipuko hiyo, rais Emmanuel Macron ambaye yuko ziarani huko Dublin amesema baada ya mkutano wake na Waziri Mkuu wa Ireland akitangaza kwamba timu za maafisa wa Ufaransa kwenye uwanja wa Kabul zinaendelea kuwaondoa mamia ya watu waliokwama karibu na uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Afghanistan.

Hii inaonyesha watu mia kadhaa walio katika hatari. Siwezi kuhakikisha kwamba tutaweza kutekeleza zoezi hili kwa sababu hali ya usalama haiko chini ya udhibiti wetu.

Kwa upande wao, Taliban "wanalaani vikali" mashambulizi haya mabaya, amesema msemaji wao, huku akisisitiza kwamba yalitokea katika eneo ambalo liko chini ya udhibii wa jeshi la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.