Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

NATO yaonya Taliban kuvamiwa ikiwa itawapa hifadhi magaidi

Taliban haipaswi kuruhusu Afghanistan iwe tena sehemu ya maficho kwa magaidi, NATO imesema leo Jumanne, ikionya kuwa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi bado ina jeshi lenye uwezo mkubwa ambalo linaiwezesha kufanya mashambulizi dhidi malengo yoyote nchini likiwa mbali.

"Tuna uwezo wa kuyashambulia makundi ya kigaidi tukiwa mbali ikiwa tutaona makundi ya kigaidi vakijaribu kujiimarisha tena na kupanga mashambulizi dhidi ya washirika wa NATO na nchi zao," amesema katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg.
"Tuna uwezo wa kuyashambulia makundi ya kigaidi tukiwa mbali ikiwa tutaona makundi ya kigaidi vakijaribu kujiimarisha tena na kupanga mashambulizi dhidi ya washirika wa NATO na nchi zao," amesema katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg. AP - Kenzo Tribouillard
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari huko Brussels, katibu mkuu wa NATO amesema kuwa "wale wanaochukua madaraka sasa wana jukumu la kuhakikisha kuwa magaidi wa kimataifa hawapati tena nafasi ya kimbilio nchini humo".

"Tuna uwezo wa kuyashambulia makundi ya kigaidi tukiwa mbali ikiwa tutaona makundi ya kigaidi vakijaribu kujiimarisha tena na kupanga mashambulizi dhidi ya washirika wa NATO na nchi zao," ameongeza Jens Stoltenberg.

Wanajeshi wa NATO pia waliondoka Afghanistan wakati wa majira ya joto, baada ya operesheni za vikosi vya nchi za Magharibi kuzindua kufuatia mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani kwa lengo la kutokomeza tishio lililotolewa na Al Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.