Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Shughuli katika uwanja wa ndege Kabul zaanza tena

Zoezi la kuondoa raia wa kigeni katika mji wa Kabul, nchini Afghanistan, limeanza tena Jumanne hii asubuhi baada ya kusitishwa kwa muda Jumatatu mchana, kwa mujibu wa afisa mmoja wa idara ya usalama kutoka nchi za magharibi.

Takriban raia watano waliuawa kwenye uwanja wa ndege Jumatatu, lakini bado haijafahamika ikiwa walipigwa risasi au walifariki katika mkanyagano.
Takriban raia watano waliuawa kwenye uwanja wa ndege Jumatatu, lakini bado haijafahamika ikiwa walipigwa risasi au walifariki katika mkanyagano. Wakil Kohsar AFP
Matangazo ya kibiashara

Uwanja wa ndege ambao ulikuwa umevamiwa siku moja kabla na maelfu ya watu wakikimbia kwa kuhofia usalama wao baada ya Taliban kuuteka mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, sasa unafanyakazi, amebaini afisa huyo.

"Watu wengi ambao walikuwepo jana wamerudi nyumbani," afisa huyo ameongeza. Shirika la habari la Reuters linasema kuwa waandishi wake wa habari walisikia milio ya risasi ikitokea upande wa uwanja wa ndege wakati hali inaonekana ni tulivu katika mji wa Kabul.

Vikosi vya jeshi vya Marekani, vinavyolinda uwanja wa ndege, wa Hamid Karzai vilisitisha safari za ndege kwa siku ya Jumatatu kutokana na kushindwa kudhibiti hali ya mambo.

Takriban raia watano waliuawa kwenye uwanja wa ndege Jumatatu, lakini bado haijafahamika ikiwa walipigwa risasi au walifariki katika mkanyagano. Afisa wa Marekani amesema watu wawili wenye silaha wanaoshukiwa kurusha risasi katika umati wa watu walipigwa risasi na kuuawa na wanajeshi wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.