Pata taarifa kuu
ISRAELI

Meli ya mafuta yashambulia Oman, wawili wauawa, Iran yashtumiwa

Iran ni mtuhumiwa mkuu wa shambulio dhidi ya meli ya mafuta katika pwani ya Oman, lililoua wafanyakazi wawili, lakini bado ni mapema sana kuwa na uhakika, vyanzo kadhaa vya Ulaya na Marekani vimesema.

Mercer Street ilishambulia Alhamisi Julai 29, 2021, hapa ilikuwa mwaka 2016 karibu na Cape Town nchini Afrika Kusini.
Mercer Street ilishambulia Alhamisi Julai 29, 2021, hapa ilikuwa mwaka 2016 karibu na Cape Town nchini Afrika Kusini. © Johan Victor/AP
Matangazo ya kibiashara

Mercer Street, meli inayotumiwa na kampuni ya Zodiac Maritime, yenye makao yake mjini London, kampuni tanzu ya kampuni ya Zodiac inayomilikiwa na kampuni ya Eyal Ofer kutoka Israeli, ilishambuliwa katika Bahari ya Arabia siku ya Alhamisi, kulingana na mmiliki wa meli hiyo, ambaye alitaja kitendo cha uharamia.

Wamiliki wa meli ya Mercer Street ni Wajapani, Zodiac Maritime ilisema Ijumaa wiki hii, na meli hiyo ilikuwa na bendera ya Liberia.

Wafanyakazi wawili, mmoja kutoka Uingereza na mwengine kutoka Romania, waliuawa, Zodiac Maritime aliongeza.

Afisa wa Israeli, aliyenukuliwa kwa sharti la kutotajwa jina na idhaa ya 13 ya Israeli, alikanusha kuwa kitendo hicho ni cha uharamia, akilaani "kitendo cha ugaidi kilichotekelezwa na Iran".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.