Pata taarifa kuu
IRAN

Tehran yaanza mchakato wa kurutubisha uranium kwa 20%

Iran  imetangaza kuanza mchakato wa kurutubisha uranium hadi 20% kinyume na sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, Tehran hata hivyo ilikuwa imejibalisha kutozidi kizingiti cha 3.67%.

Kiongozi wa kiroho wa Iran  Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei REUTERS/Caren Firouz/
Matangazo ya kibiashara

Tehran imetekeleza tishio lake kwa kuanza  kurutubisha uranium kwa 20% katika eneo la chini ya ardhi la Fordo, kulingana na msemaji wa serikali.

Kama sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, Iran iliahidi kurutubisha uranium kwa kiwango cha chini cha 4% na kwenye eneo la Natanz peke yake.

Iran inatarajia kutoa kilogramu 120 za uranium iliyorutubishwa kwa 20%. Ikikaribia kiwango cha 90% kinachoweza kutumika kwa masuala ya kijeshi.

Nchi hiyo, inaingia  katika mzunguko mpya wa mvutano na nchi za Magharibi za Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, nchi zilizotia saini kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, zilikuwa zimeiomba Iran kutotumia sheria iliyopitishwa na Bunge.

Sheria hii pia inalitaka kumalizika kwa ukaguzi ambao haukutangazwa na shirika lakimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kusitisha ukaguzi ikiwa hakuna kinachofanywa na nchi za Magharibi, hasa Marekani kuondoa vikwazo vilivyowekwa na Donald Trump dhidi ya Tehran, ambavyo vilisababisha kupunguwa kwa mauzo ya nje ya Iran na uhusiano wake wa kibenki na ulimwengu wote.

Hata hivyo, kuongeza urutubishaji wa madini ya uranium hadi asilimia 20 kumetokana na sheria iliyopitishwa na bunge la Iran mwezi uliopita baada ya kifo cha mwanasayansi mkuu wa masuala ya nyuklia nchini humo, Mohsen Fakhrizadeh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.