Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANi-DIPLOMASIA-USALAMA

Nyuklia: Iran yataka kuondolewa vikwazo vya Marekani

Iran imesema kwamba inataka vikwazo vya Marekani viondolewe kabla ya kuzindua tena makubaliano ya mwaka 2015 kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema Iran imekataa mkutano uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya juu ya makubaliano ya nyuklia ya 2015.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema Iran imekataa mkutano uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya juu ya makubaliano ya nyuklia ya 2015. ATTA KENARE AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameonesha nia yake ya kutaka nchi yake kurudi kwenye makubaliano hayo yaliyoshutumiwa mwaka 2018 na mtangulizi wake Donald Trump, kwa sharti kwamba Tehran iheshimu masharti hayo. Lakini kila upande unataka mwingine achukue hatua ya kwanza.

Nchi za Magharibizinahofu kwamba Iran inataka kupata silaha za nyuklia, lakini Tehran inahakikisha kuwa haina malengo ya kijeshi katika suala hilo.

"Utawala wa rais Joe Biden unatakiwa kubadilisha sera ya shinikizo la juu ya Trump kwa Tehran (...) Ikiwa inataka mazungumzo na Iran, lazima kwanza iiondolee vikwazo," msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa Iran, Saïd Khatibzadeh, amesema.

"Kukataa kwa utawala mpya wa Marekani kurudi kwenye makubaliano hayo ni kosa la kihistoria," ameongeza.

Washington ilisikitishwa siku ya Jumapili kukataa kwa Iran kushiriki katika mkutano usio rasmi na Marekani na nchi za Ulaya kujadili njia za kuzindua tena makubaliano haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.