Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-SIASA-USHIRIKIANO

Uchaguzi Marekani: Washington yatangaza vikwazo dhidi ya Iran

Marekani imetangaza kuchukuwa vikwazo dhidi ya kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, jeshi lenye itikadi la Tehran, pamoja na vyombo vya habari vya Irani kwa "kujaribu kuingilia" katika uchaguzi wa Marekani wa Novemba 3, licha ya Iran kukanusha madai hayo.

Mkurugenzi wa idara ya ujasusi nchini Marekani John Ratcliffe amesema kuwa maafisa wa serikali tayari walishagunduwa kwamba Iran imetuma barua pepe zinazolenga kuwatisha wapiga kura, kuchochea machafuko katika jamii na kuchafuwa jina la Rais Donald Trump.
Mkurugenzi wa idara ya ujasusi nchini Marekani John Ratcliffe amesema kuwa maafisa wa serikali tayari walishagunduwa kwamba Iran imetuma barua pepe zinazolenga kuwatisha wapiga kura, kuchochea machafuko katika jamii na kuchafuwa jina la Rais Donald Trump. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

"Utawala wa Iran umelenga mchakato wa uchaguzi wa Marekani na majaribio ya wazi ya kuchochea mgawanyiko kati ya wapiga kura kwa kueneza habari za uwongo mtandaoni ili kuwapotosha," Wizara ya Fedha ya Marekani imebaini katika taarifa

Wakati huo huo maafisa wa idara ya ujasusi ya Marekani wamesema Urusi na Iran zimetumia taarifa za wapiga kura ili kuwatisha raia wa Kimarekani pamoja na kujaribu kuwafanya wapoteze imani na mfumo wa uchaguzi.

Katika mkutano na waandishi habari juzi Jumatano, uliofanywa ghafla na kwa haraka, Mkurugenzi wa idara ya ujasusi nchini Marekani John Ratcliffe alisema Iran na Urusi ziliweza kupata baadhi ya taarifa za usajili wa wapiga kura, na kuzitumia kusambaza taarifa za uwongo kwa wapiga kura waliojiandikisha ili kuhujumu demokrasia ya nchi hiyo.

Aliongeza kwamba maafisa wa serikali tayari walishagunduwa kwamba Iran imetuma barua pepe zinazolenga kuwatisha wapiga kura, kuchochea machafuko katika jamii na kuchafuwa jina la Rais Donald Trump.

Maafisa hao hawakuweka wazi ni kwa namna gani Urusi na Iran walizipata taarifa hizo. Lakini data za usajili wa wapiga kura ni mali ya umma nchini humo na zinaweza kupatikana kiurahishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.