Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-VIKWAZO-USALAMA

Iran yaonya kwa mara nyingine kuhusu kuongezwa muda kwa vikwazo vya silaha

Rais wa Iran Hassan Rohani amesema Jumatano wiki hii kwamba Marekani "ilifanya makosa ya kijinga" kwa kujiondoa kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia na kuonya juu ya athari kubwa ikiwa washirika wake watakubali kuongeza muda kwa vikwazo vya silaha.

Rais wa Iran Hassan Rohani akiongoza mkutano wa serikali Mei 6, 2020 huko Tehran.
Rais wa Iran Hassan Rohani akiongoza mkutano wa serikali Mei 6, 2020 huko Tehran. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku kadhaa, Washington imekuwa ikishinikiza Ujerumani, Ufaransa na Uingereza (nchi hizo tatu za Ulaya zilizotia saini kwenye mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran uliofikiwa huko Vienna mwaka wa 2015) ili kupata uungwaji mkono wa kuongeza muda kwa vikwazo vya kuiuzia silaha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Vikwazo hivyo, ambavyo vitaanza kuondolewa hatua kwa hatua kuanzia mwezi Oktoba, vilipitishwa katika azimio la 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likiunga mkono mkataba wa Vienna ambao rais wa Marekani, Donald Trump alifutilia mbali, na kuamua kuiondoa nchi yake kwenye mkataba huo mwezi Mei 2018 kabla ya kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.

"Marekani ilifanya makosa ya kijinga kujiondoa kwenye mkataba huo," Rohani amesema katika mkutano wa serikali; "Jambo la busara ambalo Marekani inapaswa kufanya ni kurudi" kwenye mkataba huu, ameongeza.

Rohani amebaini kwamba kuondoa vikwazo vya silaha ilikuwa "sehemu isiyozuilika" ya mpango wa nyuklia. "Ikiwa muda wa vikwazo hivyo utaongezwa] ... wanajua vizuri ni madhara gani yanayowasubiri [...] ikiwa watafanya makosa kama hayo".

Bwana Rohani hakuelezea bayana madhara hayo, ahuku akibaini kwamba yalielezewa kwa barua iliyotumwa hapo awali kwa wahusika wengine waliotia saini kwenye mkataba huo, (Ujerumani, China, Ufaransa, Uingereza, na Urusi).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.