Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAQ-IRAN-USALAMA-USHIRIKIANO

Shambulio la Iran nchini Iraq: Askari 11 wa Marekani walijeruhiwa

Wanajeshi kumi na mmoja wa Marekani walijeruhiwa katika shambulio la Iran dhidi ya kambi ya jeshi la wanaanga ya Ain al-Assad nchini Iraq Januari 8, mwaka huu, kulingana na makao makuu ya jeshi la Marekani.

Iran ililipiza kisasi Januari 8 kwa kurusha makombora 22 ya masafa marefu katika kambi ya jeshi ya Ain al-Assad, Iraq.
Iran ililipiza kisasi Januari 8 kwa kurusha makombora 22 ya masafa marefu katika kambi ya jeshi ya Ain al-Assad, Iraq. Ayman HENNA / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kila kitu kiko sawa," rais wa Marekani amesema muda mfupi baada ya kutangazwa shambulio la Iran Januari 8.

"Hakuna Mmarekani aliyejeruhiwa katika shambulio hilo jana usiku," alisema Donald Trump siku iliyofuata katika hotuba kwenye televisheni.

"Ingawa hakuna askari wa jeshi la Marekani aliyeuawa katika shambulio la Iran la Januari 8 katika kambi ya jeshi la wanaanga ya Ain al-Assad, wengi wao walitibiwa kutokana na dalili za majeraha yaliyosababishwa na mlipuko huo na bado wanaendelea kuchunguzwa, " Kamanda Bill Urban alisema katika taarifa Alhamisi Januari 16.

"Katika siku zilizofuatia baada ya shambulio hilo, kama tahadhari, wafanyakazi wengine walisafirishwa kutoka kituo cha jeshi la wanaanga ya Ain al-Assad, nchini Iraq, hadi Kituo Kikuu cha Tiba cha Landstuhl, nchini Ujerumani; wengine walisafirishwa katika kambi ya Arifjannchini Kuwait ili kufanyiwa vipimo na uchunguzi, "amesema msemaji wa makao makuu ya jeshi la Marekani. Watu wanane walisafirishwa huko Landstuhl, na watatu katika kambi ya Arifjan, amesema msemaji huyo.

Usiku wa Januari 7 kuamkia 8, Tehran ilirusha makombora dhidi ya kambi za Ain al-Assad (magharibi) na Erbil (kaskazini), ambapo baadhi ya wanajeshi 5,200 wa Marekani wanapiga kambi, kwa kulipiza kisasi kifo cha Jenerali Iran Qassem Soleimani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.