Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Rohani atoa wito kwa majeshi ya Iran kutafuta utulivu Mashariki ya Kati

Rais wa Iran Hassan Rohani ameyatolea wito majeshi ya nchi hiyo kutafuta utulivu katika ukanda wa Mashariki ya Kati, huku akiyataka kuwa makini kutokana na "uchokozi," televisheni ya serikali imeripoti

Rais wa Iran Hassan Rohani katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Februari 16, 2020.
Rais wa Iran Hassan Rohani katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Februari 16, 2020. Official Presidential website/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wito huo unakuja wakati vita vya maneneo vinaendelea kuongezeka kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani.

Siku ya Alhamisi mkuu wa majeshi ya mapinduzi alionya kwamba Iran "itaangamiza" chombo chochote cha kivita cha Marekani ambacho ni tishio kwa usalama wake katika maji ya Ghuba, siku moja baada ya tishio kama hilo kutoka kwa Rais wa Marekani, Donald Trump.

"Tunapaswa kufuatilia kwa uangalifu mikakati inayohakikisha utulivu wa kudumu katika kanda hii, huku tukiendelea kuwa makini na kuepo katika eneo hilo," Hassan Rohani amemwambia Waziri wa Ulinzi Amir Hatami katika mahojiano ya simu, kulingana na taarifa iliyotolewa na televisheni ya serikali ya Iran.

Mvutano kati ya Washington na Tehran umeongezeka tangu Donald Trump alipoamua Mei 2018 kuiondoa Marekani kwenye mkataba wa mpango wa nyuklia wa Irani wa mwaka 2015 na kurudisha kuchukuwa vikwazo dhidi ya Iran.

Uhasama kati ya nchi hizo mbili ulisababisha mashambulizi ya kijeshi mapema Januari, huku Iran ikirusha makombora dhidi ya kambi za jeshi Marekani nchini Iraq kwa kulipiza kisasi mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani aliyeuawa na shambulio la jeshi la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.