Pata taarifa kuu
IRAN-AFYA-CORONA

Coronavirus: Visa vya maambukizi vyaendelea kuongezeka Iran

Mamlaka nchini Iran imetangaza vifo vipya 138 vinavyohusiana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, na kufikisha idadi ya vifo kufikia zaidi ya 3,000.

Afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Irani lakifanya vipimo kwa abiria wa teksi, Machi 26, 2020, karibu na Tehran.
Afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Irani lakifanya vipimo kwa abiria wa teksi, Machi 26, 2020, karibu na Tehran. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Iran ni mojawapo ya nchi zinazoathirika zaidi na virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona).

Katika muktadha huu wa janga hilo, rais wa Iran Hassan Rohani kwa upande wake amebaini kwamba Marekani imekosa "nafasi ya kihistoria" ya kuondoa vikwazo vyake dhidi ya Tehran.

Iran imrthibitisha rasmi jumla ya vifo 3,036 vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid-19 na visa vipya 2,987 vya maambukizi ndani ya saa 24 yaliyopita, na kufikisha jumla ya visa vilivyothibitishwa 47,593 vya maambukizi, amesema Kianouche Jahanpour, msemaji wa Wizara ya Afya wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao.

Hassan Rohani amesema kuwa watu 15,473 waliolazwa hospitalini wamepona.

Akizungumzia ugonjwa huo, Bwana Rohani alikuwa amekosoa Marekani hapo awali, akibaini kwamba nchi hiyo imekosa "nafasi ya kihistoria (...) kwa kudanganya, ikisema kuwa haina chuki na raia wa Iran.

"Marekani "haikujifunza chochote hata wakati wa hali hii ngumu duniani (...). Ilikuwa ni swali la kibinadamu. Hakuna mtu ambaye angeishutumu kwa kurejelea" msimamo wake, rais wa Iran amesema wakati wa mkutano wa serikali uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Rais wa Marekani, Donald Trump alijiondoka mwenyewe kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran mwezi Mei 2018, na aliichukulia Iran vikwazo vikali vya kiuchumi, ambavyo vilenga hasa sekta ya mafuta na benki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.