Pata taarifa kuu
DUNIA-CORONA-AFYA

Virusi: Ulimwengu wakabiliwa na janga baya zaidi tangu mwaka 1945, watu 30,000 wafariki Ulaya

Ugonjwa wa Covid-19 (Corona) umeuwa zaidi ya watu 30,000 huko Ulaya na janga hilo, ambalo Umoja wa Mataifa umelitaja kama mgogoro mbaya zaidi ambao umewakumba binadamu tangu mwaka 1945, sasa unatishia kuiathiri zaidi Marekani.

Ulimwenguni kote, mgogoro huu wa kiafya pia unaendelea kusababisha majanga, ambapo watu 41,000 wamefariki dunia, kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP.
Ulimwenguni kote, mgogoro huu wa kiafya pia unaendelea kusababisha majanga, ambapo watu 41,000 wamefariki dunia, kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya theluthi mbili ya waathiriwa wa Ulaya ni kutoka Italia na Uhispania, kulingana na tathmini iliyotolewa na shirika la habari la AFP kutoka vyanzo rasmi Jumatano wiki hii saa 7:00.

Ulimwenguni kote, mgogoro huu wa kiafya pia unaendelea kusababisha majanga, ambapo watu 41,000 wamefariki dunia, kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP.

Tangu kuzuka kwa janga hilo nchini China mwezi Desemba, zaidi ya visa 830,000 vya maambukizi vimetangazwa rasmi ulimwenguni kote, zaidi ya nusu ya visa hivyo vimeripotiwa Ulaya, 186,000 nchini Marekani na zaidi ya 108,000 huko Asia.

Ili kukabiliana dhidi ya kusambaa kwa janga hili, zaidi ya watu bilioni 3.6, au asilimia 46.5 ya watu ulimwenguni kote, wametakiwa kukaa nyumbani.

Nchini China, wakati marufu ya kutoka nje imeanza kuondolewa hatua kwa hatua huko Wuhan, ambako ugonjwa huo ulianzia, hatua za kwanza zimewataka wakazi wa mji huo kuweka kwenye kaburi za mawe masanduku yaliyojaa majivu ya wapendwa wao.

Wakati huo huo nchi mbalimbali zimeendelea kuchukuw ahatua za kukabiliana dhidi ya kusambaa kwa virusi vya Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.