Pata taarifa kuu
URUSI-ISLAMIC STATE

Jeshi la Urusi lasema limewauwa viongozi na wapiganaji wa Islamic State

Jeshi la Urusi limesema liliwashambulia viongozi wa kundi la Islamic State nchini Syria mwezi uliopita na sasa linathibitisha ikiwa lilimuua kiongozi wa kundi hilo Abu Bakr al-Baghdadi.

Ndege ya kivita ya Urusi inayotekeleza mashambulizi nchini Syria
Ndege ya kivita ya Urusi inayotekeleza mashambulizi nchini Syria intelligencebriefs.com
Matangazo ya kibiashara

Aidha jeshi hilo  limesema, wanajeshi wake wakitumia ndege za kivita aia ya Sukhoi, walitumia dakika 10 kutekeleza mashambulizi ya angaa katika ngome ya viongozi hao karibu na mji wa Raqa tarehe 28 mwezi uliopita.

Makamanda wa juu wa jeshi la Urusi wamesema wanaamini kuwa waliwauwa makanda 30 wa kundi hili na wapiganaji wake 300.

Ripoti zinasema  shambulizi hilo lilifanyika wakati Abu-Bakr al-Baghdadi akiongoza mkutano akiwa na  makanda wake na  wapiganaji wa kundi hilo.

Urusi imesema tayari imeshaiambia Marekani kuhusu shambulizi hili na wanashirikiana kubaini taarifa zaidi.

Rais Vladimir Putin alituma jeshi la nchi yake kwenda  Syria mwaka 2015, kuisaidia na jeshi la nchi hiyo kuyashinda makundi ya waasi kama Islamic State.

Hata hivyo, operesheni yake hivi karibuni imeendelea kuibua mashaka baada ya kudaiwa kuwa mashambulizi ya jeshi lake yanawalenga raia wasiokuwa na hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.