Pata taarifa kuu
MISRI-ISRAEL-PALESTINA

Rais wa Misri aomba kuahirishwa kwa kura ya UN juu ya makaazi ya Waisrael

Kwa ombi la Misri Alhamisi hii, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuahirisha kura rasimu ya azimio linalodai Israel iachane na shughuli zake ukoloni. Ofisi ya rais wa Misri imetangaza Ijumaa kwamba ombi hilo lilitolewa baada ya mazungumzo ya simu kati ya rais Abdel Fattah al-Sissi na rais mteule wa Marekani, Donald Trump. Viongozi hao wawili walikubaliana kuupa utawala wa Trump nafasi ya kusimamia kesi hiyo.

Rais wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi akiomba kuahirishwa kwa kura ya UN juu ya makaazi ya Waisrael .
Rais wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi akiomba kuahirishwa kwa kura ya UN juu ya makaazi ya Waisrael . Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mapema Alhamisi jioni rais mteule wa Marekani aliomba nchi yake kutumia kura yake ya turufu kwenye rasimu ya azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya makaazi ya Waisrael katika Jerusalem ya Mashariki.

Marekani imekuwa ikiunga mkono Israel katika Umoja wa Mataifa, lakini wanaounga mkono azimio hilo wamekuwa wakiamini kwamba utawala wa rais Obama utasusia kura hiyo.

"Kama Marekani inavyosema kwa muda mrefu, amani kati ya Waisrael na Wapalestina inaweza kupatikana tu kutoka mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili, na wala si kwa njia ya masharti yanayotolewa na Umoja wa Mataifa," alisema rais mteule wa Marekani. "Marekani inapaswa kutumia kura yake ya turufu kwenye azimio lililojadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa," Bw Trump aliomba, wakati ambapo kura ilikua inatarajiwa Alhamisi hii saa 9h alaasiri mjini New York. Rasimu ya azimio inadai kwamba Israel iache shughuli zake za ukoloni katika maeneo ya Palestina na katika Jerusalem ya Mashariki.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump alilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuishawishi Israel kusitisha ujenzi wa makaazi ya Israel katika ardhi ya Palestina.

Katika taarifa iliotolewa kabla ya kura hiyo, Bw Trump alisema kuwa amani haitaafikiwa kupitia hatua ya Umoja wa Mataifa kwa kuweka masharti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.