Pata taarifa kuu
SYRIA-MAPIGANO

Syria: Waasi wajaribu kupata mafanikio Aleppo

Hali katika mji wa Aleppo imeendelea kuwa ya wasiwasi, Jumapili, Agosti 7, kufuatia kusonga mbelea kwa muungano wa wanajihadi na waasi. Ndege za Syria na Urusi ziliendelea kuzidisha mashambulizi kwa kuwazuia waasi kusonga mbele.

Wapiganaji wa wa kijihadi wa kundi la Fateh al-Sham Front, zamani Al-Nosra, kusini mwa jimbo la  Aleppo, Agosti 5, 2016.
Wapiganaji wa wa kijihadi wa kundi la Fateh al-Sham Front, zamani Al-Nosra, kusini mwa jimbo la Aleppo, Agosti 5, 2016. REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wanajaribu kuimarisha ngome zao. Katika maeneo ya ya magharibi mwa jimbo la Aleppo, ambayo yanadhibiitiwa na serikali na kuzingirwa sehemu moja na jeshi la serikali wakazi wa maeneo hayo wana hofu ya kukabiliwa na uhaba wa chakula na maji safi.

Jeshi la Syria na washirika wake Iran na wapiganaji wa Hezbollah kutoka Lebanonwanajaribu jaribu kupunguza hasara walizozipata hivi karibuni. Waasi, kwa upande wao, wanajaribu umuhimu wa mafanikio mafanikio yao waliyoyapata.

Barabara ya uliyofunguliwa na wanajihadi kuelekea meneo ya mji wa Aleppo haijakua salama. Ni vigumu kusafirisha chakula kwa kutumia barabar hiyo . Wakati huo huo, maeneo yanayokaliwa na wafuasi wa serikali, ambapo wanaishi mamilioni ya raia, ni vigumu kuingiza chakula.

Jeshi la Syria limesema kuwa limepata njia mbadala kwa kusafirisha chakula na mafuta, lakini barabara hii ni hatari kama ile inayotumiwa na waasi.

Ndege za Syria na Urusi zilishambulia, Jumapili hii, Agosti 7, shule za kijeshi zilizotekwa na waasi siku moja kabla magharibi mwa jimbo la Aleppo. Chuo cha kijeshikiliteketezwa kwa mabomu yaliyodondoshwa na ndege. Hata hivyo utawala wa Bashar Al Assad umeshindwa kuwasogeza nyuma waasi, ambao hata wao wameshindwa kuimarisha ngome zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.