Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-MAPIGANO

Syria: ndege za Urusi zawakwanisha waasi karibu na Aleppo

Jumanne hii, ndege za Urusi zinazosaidi majeshi ya serikali ya Syria zimewakwamisha waasi kwa mashambulizi makali ya anga kusini mwa mji wa Aleppo. Waasi walianzisha mashambulizi katika mji huo ili kufungua baadhi ya maeneo ya mji huo yanayozingirwa na vikosi vya serikali. Mji wa Aleppo unakabiliwa na vita kwa miaka kadhaa sasa.

Askari wa jeshi la Syriakatika eneo la kusini ya barabara ya mjini Castello, Julai 28, 2016.
Askari wa jeshi la Syriakatika eneo la kusini ya barabara ya mjini Castello, Julai 28, 2016. Reuters/Sana
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Syria (OSDH), mashambulizi yaliyoendeshwa Jumapili ni makubwa kuwahi kufanywa na waasi wanaoshikilia mji wa Aleppo tangu yale ya mwaka 2012 ambayo yalipelekea kuteka nusu ya mji mkuu wa kaskazini mwa Syria na kuweza kuutikisha utawala wa Bashar al-Assad.

Lengo la mashambulizi ya waasi ni kufungua njia mpya kwa kuweza kupitisha misaada ya chakula na vifaa vya kijeshi kwa kukuviingiza mashariki ya mji na kuzuia utawala wa Assad kuliteka jiji zima, linalokabiliwa na changamoto kubwa ya mgogoro tata ambao unaiathiri Syria tangu mwaka 2011.

Aleppo imegawanywa tangu mwezi Julai mwaka 2012 kati ya maeneo ya magharibi yaliyo mikononi mwa serikali na maeneo yanayodhibitiwa na waasi na kuzingirwa na jeshi tangu Julai 17.

Katika vita hivi, utawala unaungwa mkono na kikosi cha anga cha Urusi, na nchi kavu majeshi ya serikali yanasaidiwa na wapiganaji wa Iran na wale wa Hezbollah kutoka Libanon, kwa mujibu wa OSDH. Waasi wanaungwa mkono na wanajihadi wa kundi la al-Sham Fateh Front (kundi la zamani la Al-Nosra Front, ambalo lilikata mahusiano na Al Qaeda).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.