Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MAPIGANO

Zaidi ya watu 60 wauawa katika mashambulizi ya muungano

Nchini Syria, zaidi ya watu 60, wakiwemo watoto, wameuawa Jumanne hii katika mashambulizi ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani karibu na kijiji kinachodhibitiwa na wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS) katika jimbo la Aleppo, kwa mujibu washirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH).

Vikosi vya usalama vya Syria vikiwaokoa wafanyakazi wa hopitali ya Muhafaza Aleppo, baada ya waasi kurusha risasi, Mei 3 2016.
Vikosi vya usalama vya Syria vikiwaokoa wafanyakazi wa hopitali ya Muhafaza Aleppo, baada ya waasi kurusha risasi, Mei 3 2016. GEORGE OURFALIAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mji mkuu wa mkoa huu wa kaskazini mwa Syria, kundi kubwa la waasi wa Kiislamlimetangaza kwamba linaanza "vita" vyenye lengo la kuvunja vizuizi vilivyowekwa na vikosi vya serikali hivi karibuni katika maeneo ya waasi.

Eneo la mashariki ya Aleppo, linalodhibitiwa na wapiganaji, limeendelea kulengwa na mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa Jumanne hii, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Kilomita 100 kutoka mji wa Aleppo, ndege za muungano ziliendesha mashambulizi mapema alfajiri wakati ambapo raia walikua wakiyakiyakimbia mapigano katika kijiji cha al-Toukhar karibu na ngome ya wanajihadi ya Minbej, amesema Rami Abdel Rahman, Mkurugenzi wa OSDH.

"Kwa uchache watu 56 wameuawa, wakiwemo watoto 11 na wengine kadhaa waliojeruhiwa, baadhi wakijeruhiwa vibaya," alimesema Bw Abdul Rahman.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.