Pata taarifa kuu
SYRIA-MAPIGANO

Waasi wakabiliwa na mashambulizi ya jeshi la serikali Aleppo

Katika wiki za hivi karibuni, jeshi la serikali ya Syria limeendelea kujidhatiti katika makuu yake mjini Aleppo. Jumapili iliyopita, makundi ya waasi yalianzisha mashambulizi bila mafanikio kwa sasa. 

Mapigano yaendelea kushuhudiwa katika jimbo la Aleppo, Syria.
Mapigano yaendelea kushuhudiwa katika jimbo la Aleppo, Syria. REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), makundi ya waasi yamepoteza katika siku za hivi karibuni baadhi ya maeneo waliokua wakishikilia tangu mwanzo wa mashambulizi yao Jumapili iliyopita. Usiku wa kuamki Alhamisi hii, kwa uchache watu 10 wakiwemo watoto wanne, waliuawa katika mashambulizi ya waasi katika maeneo yanayokaliwa na watu wanaounga mkono utawala wa Bashara Al-Assad katika jimbo la Aleppo, kwa mujibu wa OSDH. Tangu Jumapili, zaidi ya raia 40 waliuawa katika mashambulizi katika jimbo la Aleppo.

Lengo muhimu la mashambulizi hayo ya waasi ilikuwa kuliteka eneo la serikali la Ramoussa, kusini magharibi mwa jimbo la Aleppo, ambapo udhibiti wa eneo hilo ungeweza kuruhusu waasi kufungua njia kwa kupeleka chakula na vifaa vya kijeshi katika maeneo yao ya mashariki vitongoji yao. Magari yanayosafirisha chakula cha jeshi na raia katika eneo la magharibi mwa jimbo la Aleppo yanapita katika eneo hilo la Ramoussa.

Kwa upande wa wapiganaji, makundi kadhaa yenye silaha yanashiriki katika vita, ikiwa ni pamoja Front al-Sham Fatah kundi la zamani la Al-Nosra Front, ambalo hivi karibuni lilitangaz kujitenga na al-Qaeda. Upande wa serikali, wanajeshi wa serikali wanasaidiwa na jeshi la anga la Urusi na nchi kavu linasaidiwa na vikosi vya Iran na wapiganaji wa Lebanon wa Hezbollah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.