Pata taarifa kuu
Wimbi la Siasa

Wakaazi wa GOMA mkoani Kivu kaskazini wapinga utovu wa usalama mashariki ya DRC

Imechapishwa:

Makala ya wimbi la siasa inaangazia maandamano ya mamia ya waakazi wa mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakipinga utovu wa usalama na ripoti kuwa, serikali nchini humo imeingia kwenye makubaliano na nchi jirani ya Rwanda, kutuma  polisi wake, kulinda usalama mjini Goma. Katika siku za hivi karibuni hasa mjini Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kumeshuhudiwa visa vya watu kuvamiwa, kutekwa nyara na kuuawa akiwemo mwanaharakati wa Lucha.Wakati wa maandamano hayo wiki hii, kuliropitiwa kuuawa kwa watu wanne, akiwemo afisa wa polisi na mtoto, baada ya kutokea kwa makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama. Kuelewa nini chanzo cha utovu wa usalama katika eneo hilo, ungana na mwandishi wetu Victor Abuso

Jiji la Goma katika mkowa wa Kivu kaskazini Mashariki ya DRC, 2017
Jiji la Goma katika mkowa wa Kivu kaskazini Mashariki ya DRC, 2017 © Ruben Lukumbuka/RFI Kiswahili
Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.