Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

MONUSCO yaongezwa mwaka mmoja kuendelea kuhudumu DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeuongezea muda wa wa mwaka mmoja Ujumbe wake nchini DRC (MONUSCO) na kuwataka walinda amani kuelekeza nguvu zao Kaskazini-Mashariki mwa nchi, huku likisisitizia kufanyika kwa operesheni za pamoja na vikosi vya nchi hiyo, FARDC.

Walinda amani wa MONUSCO wakishika doria katika mitaa ya Goma, DRC, Machi 19, 2020.
Walinda amani wa MONUSCO wakishika doria katika mitaa ya Goma, DRC, Machi 19, 2020. REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha hapo jana Baraza hilo limejadili mapendekezo kadhaa yaliyochapishwa katika azimio nambari 2612 yaliyoandaliwa na Ufaransa kabla ya kupitishwa kwa kauli moja na wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mojawapo ya kipengele kilichojadiliwa kwa undani wake ni kwamba hadi Desemba 20 mwaka 2022 Monusco itakuwa imehakikisha imebaki na wanajeshi 14,160 na maafisa wa polisi 2,001.

Wanajeshi wake wa kulinda amani walioko mkoani Tanganyika kusini-mashariki mwa nchi, wataondolewa katikati ya mwaka wa 2022 na kuunganishwa na vikosi vya Umoja huo huko Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, majimbo matatu ambayo yanaendelea kushuhudia kuzorota kwa hali ya usalama kufuatia kuwepo kwa makundi yenye silaha.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limesema ipo haja ya kuheshimiwa kwa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu, na sasa limesisitizia suala la kushirikishwa katika operesheni za pamoja za vikosi vya jeshi la Congo FARDC, ikiwa ni pamoja na brigedi yake ya kuingilia kati.

Azimio hili linakuja wakati ambapo jeshi la Uganda limekuwa likifanya operesheni za kijeshi na FARDC tangu Novemba 30 dhidi ya waasi wa ADF, ambao wamekuwa wakiua raia na kuchoma miji na vijiji ikiwemo magari, mashariki mwa Nchi hiyo.

Majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri yamekuwa katika hali ya dharura na kuzingirwa tangu mwezi Mei, huku mauaji yakiendelea kuripotiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.