Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Habari za uongo kuwa rais wa Uganda amefariki baada ya kuambukizwa Korona

Imechapishwa:

Siku kadhaa baada ya rais wa Uganda Yoweri Museveni kuthibitisha kuambukizwa Uviko 19, mnamo Juni 7 mwaka 2023, ripoti kwenye mitandao ya kijamii ilisambazwa ikidai kuwa hali yake ya kiafya imedhofika zaidi na kwamba alikuwa amelazwa hospitalini na baadae aliaga kutokana na changamoto za maambukizi hayo.

Taarifa za uongo kuwa rais wa Uganda amefariki baada ya kuugwa uviko 19
Taarifa za uongo kuwa rais wa Uganda amefariki baada ya kuugwa uviko 19 © rfi
Matangazo ya kibiashara

Ukweli ni kuwa Museveni mwenye umri wa miaka 78, alikuwa amejitenga kwa zaidi ya wiki moja, wala hakuwa amefariki, na hili lilidhihirika alipohutubia bunge la Uganda.

Wakati baadhi ya machapisho kwenye mitandao ya kijamii yakitangaza kuwa Museveni amefariki, wengine walikuwa wakihoji iwapo uvumi huo ni wa kweli. Mfano huyo hapa aliandika hivi , "Je ni kweli huyu Museveni amefariki au nasikia mambo yangu?" Hii ilichapishwa kutoka Kenya, kwa vile ina bendera ya kenya.

"Pia niliona baadhi ya watu wachache kutoka, nadhani, Kenya, wakisema kwamba nilikuwa ICU nk. Kama ningekuwa ICU, serikali ingeijulisha nchi. Kuna nini cha kuficha?" aliandika kwenye tweet ya Juni 13, 2023.

Mnamo Juni 15, Museveni kupitia mtandaoni alihutubia bunge la Uganda wakati wa kuwasilishwa wa bajeti ya nchi hiyo.

Taarifa hizo zilikuwa ni za uongo tu maana rais Museveni yuko hai.

Vipindi vingine
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:16
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.