Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

DRC: Ubelgiji unamuondoa balozi wake jijini Kinshasa: Sio Kweli

Imechapishwa:

Nchini DRC, ambapo ujumbe umekuwa ukienea kwenye makundi ya mitandao ya kijamii ukidai kwamba Ubelgiji inapanga kumuita balozi wake nchini humo kurejea nyumbani, na aliyetangaza hilo ni Didier Reynders. Didier Reynders ni kamishna wa Umoja wa Ulaya kuhusu sheria.

Taarifa za kupotosha nchini DRC kwamba Ubelgiji imesema inamuondoa balozi wake jijini Kinshasa
Taarifa za kupotosha nchini DRC kwamba Ubelgiji imesema inamuondoa balozi wake jijini Kinshasa © FMM
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa, Kongo inapitia kipindi kigumu katika historia yake ikiwemo uchumi unaoyumbayumba, kuendelea kudorora kwa usalama, mgogoro wa kisiasa na vyote hivi vinaendelea chini ya uongozi wa rais Tschisekedi.

Madai zaidi yanasema kuwa raia wa Kongo wanaamini kuwa maslahi yao hayaangaziwi kwa sasa, na rais Tschisekedi hana udhibiti wa nchi kutokana na yeye kukosa tajriba na uwezo wa kutimiza ahadi zake.

Sehemu ya maandishi inasema Ubelgiji inajitolea kuheshimu haki za wanawake wa Kongo na kutangaza kukasirishwa kumuunga mkono rais ambaye anatumia muda mwingi katika saluni za Ulaya kuliko kuendeleza nchi yake."

Baadhi ya mambo tuliyogundua katika chapisho hili; jina la balozi halijatajwa, jina la rais wa DRC limeandikwa moja tu, Tschisekedi, na mskilizaji katika barua rasmi majina yote hutumika.

Sisi kama RFI Kiswahili, tuliandika barua pepe kwa ubalozi wa Ubelgiji huko Kinshasa, ili kubainisha taarifa hii na jibu tulilopata ni hili. “Tunathibitisha kuwa habari hii ni ya uongo.”

Vipindi vingine
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:16
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.