Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Tume inayosimamia matumizi ya nguvu za atomiki yaitaka Iran kuweka wazi maswala yote ya mpango wake wa Nyuklia yanayotiliwa mashaka

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia matumizi ya nguvu za Atomiki AIEA Yukiya Amano, ameishinikiza serikali ya Iran kuweka bayana maswala yote yanayotiliwa mashaka na mataifa ya magharibu kuhusu mpango wa Nyuklia unaozaniwa kuwa na malengo ya kijeshi.

yukiya Amano Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia matumizi ya nguvu za Atomiki
yukiya Amano Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia matumizi ya nguvu za Atomiki REUTERS/Heinz-Peter Bader
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya iran imeonyesha nia nzuri ya kushirikiana na nchi zenye nguvu duniani katika kutafuta suluhu ya kumaliza mzozo huu, lakini bado kuna mambo mengi ya kufanya katika kutatua maswali nyeti yaliowekwa kipolo.

Yukiya Amano ambaye ni raia wa wa Japani anaona kwamba kuna umuhimu mkubwa kwa Irab kuweka wazi maswali yote yanayo tatanisha hususan uwezekana wa matumizi ya mpango huo kijeshi na utekelezwaji wa ptotokali iliosaniwa, ambayo inaagiza uchunguzi wa mara kwa mara wa AIEA.

Hapo jana rais wa Iran Hassan Rohani aliyatuhumu mataifa ya magharibi kwa kulenga kuchelewesha mpango wake wa nyuklia. Rais Rohani amesema katika hotuba yake iliopeperushwa kenye luninga ya taifa nchini Iran kwamba, AIEA ilifanya ukaguzi wa muda mrefu katika viinu vya nyuklia ya Iran na kuarifu kuw ahakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa mpango huo ni wa kijeshi.

AIEA ilichapisha ripoti mwezi Novemba mwaka 2011 iloonyesha kuwa mapngo wa Iran unalenga kutengeneza bomu la atomiki, jambo ambalo limeendelea kukanushwa na serikali ya Iran

Swala hilo la malengo ya kijeshi halikujadoiliwa kwa kina katika makubaliano yenye pointi saba yaliotiwa sahihi mwaznoni mwa mwezi Februari ambapo Iran ilikubali kutowa maelezo kuhusu vifaa vinavyotumiws kwa kulipua bomu.

Majadiliano ya AEIA yanafanyika tofauti na yale yanayoendeshwa na mashirika matano yenye nguvu duniani lakini yote yana lengo moja. Mwezi Novemba 24 iliopita Iran na mataifa 5+1 ikiwa ni pamoja na (Marekani, Ufaransa, Uingereza, Urusi, China na Ujerumani) yalifikia makubaliano ya mpango wa miezi sita ambapo Iran ilikubali kupunguza urutubishwaji wa Nyuklia huku mataifa hayo yakikubali kupunguza vikwazo. Mkataba huo unatekelezwa tangu Januari 20 mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.