Pata taarifa kuu
UGANDA-BOBI WINE

Bobi Wine asitisha kwa muda kampeni zake za uchaguzi

Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ametangaza kusitisha kampeni zake za uchaguzi kwa muda ili aende tume ya uchaguzi kupata maelezo kuhusu ni nani anayesimamia kampeni za Uchaguzi Mkuu mwezi Januari mwakani.

Ugandan pop star and government critic Bobi Wine freed on bail
Ugandan pop star and government critic Bobi Wine freed on bail France24
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya mwanasiasa huyo imekuja baada ya wafuasi wake kujeruhiwa Jumanne wiki hii wakati maafisa wa usalama walipowarushia mabomu ya kutoa machozi katika eneo la Kayunga, karibu na mji wa Kampala.

Akiendelea na kampeni zake, maofisa wa jeshi na polisi walifyatulia risasi gari lake na kuharibu vioo pamoja na magurudumu yakem huku watuj kadhaa wakijeruhiwa na wengine kunusurika kifo.

Wiki mbili zilizopita, watu 54 walipoteza maisha kufuatia maandamano ya kudai Bobi Wine aachiwe huru baada ya kukamatwa kwa madai ya kukiuka masharti ya watalaam wa afya kuhusu kampeni zake kutokana na hofu ya kusambaza virusi vya Corona.

Makabiliano kati ya wafuasi wa mwanamuziki huyo maarufu na vikosi vya usalama vya Uganda yaeendelea kuripotiwa hapa na pale na tayari rais Yoweri Kaguta Museveni, hivi karibuni alionya kwa wale wanaotaka kuhatarisha usalama wa nchi kwamba wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria za Uganda.

Mamlaka nchini humo winatarajiwa kumtaki Bobi Winem mahakamani kwa makosa ya kuhatarisha usalama na kusambaza maambukizi ya Covid 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.