Pata taarifa kuu
CUBA-KENYA-USALAMA

Cuba yakanusha habari za kuachiliwa kwa raia wake wawili Kenya

Cuba imekanusha ripoti kuhusu kuachiiliwa kwa madaktari wake wawili, waliotekwa na wanamgambo wa  Al-Shabaab mwaka wa  2019 Kaskazini Mashariki mwa Kenya na kundi la wamechiliwa huru.

Mji wa Madera, umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya kundi la Al shabab kutoka Somalia.
Mji wa Madera, umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya kundi la Al shabab kutoka Somalia. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka katika wizara ya mambo ya nje ya cuba,wawili hao  Assel Herrera Correa na Landy Rodriguez Hernandez, bado wanazuiwa,

Jumatano ya wiki hii, afisa wa polisi wa ngazi ya juu nchini Kenya alikuwa amethibitishia shirika la habari la AFP kuwa mateka hao walikuwa wameachiliwa huru.

Assel Herrera na Landy Rodriguez walitumwa Mandera, kaskazini mwa Kenya, karibu na mpaka wa Somalia mwaka 2018.

Mwezi Aprili 2019, wakati walikuwa njia kuelekea kazini, madaktari hao walitekwa nyara na wanamgambo wa kundi kutoka Somalia la Al Shabab. Mlinzi aliuawa wakati wa utekaji nyara.

Madaktari hao wawili walikuwa sehemu ya kundi la wataalamu 100 wa afya wa Cuba waliotumwa nchini Kenya mwezi Juni 2018 baada ya makubaliano ya afya yaliyosainiwa kati ya Nairobi na Havana.

Miongoni mwa madaktari waliokuwa kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa x-ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva.

Wamekuwa wakitoa huduma na kushauriana na madaktari wengine katika maeneo tofauti nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.