Pata taarifa kuu
SOMALIA-KENYA-AL SHABAB-USALAMA

Somalia: Mapigano yazuka Jubaland kwenye mpaka na Kenya

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne hii asubuhi, Umoja wa Mataifa umesema watu 56,000 wamelazimika kuyatoroka makazi yao nchini Somalia kwa sababu ya mvutano katika Jimbo linalojitawala la Jubaland.

Jimbo linalojitawala la Jubaland, Kusini mwa Somalia.
Jimbo linalojitawala la Jubaland, Kusini mwa Somalia. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zote kupunguza hasara kwa raia, shule, nyumba na vituo vya afya.

Mapigano yaliyozuka Jumatatu (Machi 2) kati ya jeshi la Somalia na vikosi kutoka Jubaland, moja wapo ya majimbo yanayojitawala nchini Somalia, yalisababisha raia wengi wanaingiliwa na wasiwasi mkubwa kwenye jimbo hilo lililo kwenye mpaka na Kenya. Mpaka sasa haijafahamika hasara iliyotokea iwe kwa upande wa raia na mali. Hali hiyo ilizua hofu kwa wakazi wa pande zote mbili za mpakani, na kusababisha haki ya kutoamniniana kati ya Nairobi na Mogadishu.

Kwa majuma kadhaa, jeshi la Somalia limekuwa likiingiza kwa wingi vikosi vyake katika mkoa wa Balad Hawo, ulio chini ya himaya ya Jubaland. Wiki iliyopita katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani pia ilisema ni jambo "lisilokubalika" kuwapo kwa askari wa rais wa Somalia Farmajo katika mkoa huo.

Mogadishu inasema inaimarisha usalama kwenye mpaka wake na Kenya. Lakini wengi wanashuku serikali kuu ya Mogadishu inataka, kwa gharama zote, kumdhibiti waziri wa zamani wa usalama wa Jubaland, Abdirashid Janan. Alikamatwa mnamo mwezi Oktoba na kuletwa Mogadishu, Lakini alitoroka kutoka jela mwezi Januari mwaka huu.

Tatizo ni kwamba ofisa huyo alipata hifadhi ya ukimbizi katika mji wa mpaka wa Kenya wa Mandera, mita mia chache kutoka mahali ambapo vurugu zilianza jana Jumatatu.

Jubaland na Kenya ni washirika. Vikosi vya Kenya vilisaidia sana mkoa huo kuwatimua wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Al Shabab. Uhusiano huu kati ya Jubaland na Kenya unaisumbua serikali kuu ya Somalia.

Kumekuwa na mazingira ya kutatanisha, tangu mwaka moja sasa kati ya Somalia na Kenya, kwa sababu ya mzozo wa mpaka wa bahari. Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili jirani bado yanasuasua, wakati siku chache zilizopita, wabunge kumi na mmoja kutoka kaskazini mwa Kenya walikwenda kumwona Rais wa Somalia Farmajo, hali ambayo ilisababisha serikali ya Nairobi kupata hasira.

Kwa vyovyote vile, licha ya hali hiyo, wataalam wanabaini kwamba mivutano hii itawapa nguvu tena magaidi wa Al Shabab .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.