Pata taarifa kuu
SOMALIA-KENYA-AJALI-USALAMA

Somalia, Kenya waahidi kushirikiana katika uchunguzi kuhusu ajali ya ndege ya mizigo

Baada ya kutokea kwa ajali ya ndege ya mizigo iliyokuwa ikisheheni msaada wa vifaa Kusini magharibi mwa Somalia Jumatatu wiki hii, na kugharimu maisha ya watu sita waliokuemo katika ndege hiyo Somalia na Kenya wameahidi kushirikiana kwa uchunguzi.

Eneo la ajali ya ndege iliyotokea karibu na mji wa Bardale, Somalia, Mei 4, 2020.
Eneo la ajali ya ndege iliyotokea karibu na mji wa Bardale, Somalia, Mei 4, 2020. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Miili ya watu wanee, raia wa Kenya iliiwasili nchini Kenya Alhamisi wiki hii.

Marais wa nchi hizo mbili (Kenya na Somalia) wameahidi kushirikiana ili kutoa mwanga kuhusu sababu za ajali hiyo, ambayo bado haijajulikana.

Licha ya tofauti zao, lakini siku moja baada ya ajali hiyo, Jumanne asubuhi, Rais wa Somalia alimuita mwenzake wa Kenya. Mohammed Abdullah Farmajo kwanza alitoa salamu za rambirambi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuwapoteza kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Africa Express Airways. Kisha aliitaka mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya kushiriki katika uchunguzi unaoendeshwa na Somalia ili kubaini sababu ya ajali hiyo.

Siku ya Jumatano, maafisa wa Somalia, Kenya na wale kutoka Ethiopia walizuru eneo la ajali, karibu na uwanja wa ndege wa Bardale. Akisindikizwa na waandishi wa habari, Waziri wa Uchukuzi wa Somalia hakutaka kutaja sababu za janga hilo. Alibaini tu kwamba jeshi la Umoja wa Afrika, Amisom, ndilo linadhibiti eneo la anga (angahewa), askari wa Ethiopia na Somalia ndio wanadhibiti uwanja wa ndege wa Bardala, na kwamba wanamgambo wa Al Shabab pia wanaendesha vitendo vyao katika msitu unaozunguka uwanja wa ndege.

Ushuhuda uliotolewa na vyombo vya habari vya nchini Somalia unaonyesha kwamba ndege hiyo ilidunguliwa kwa maroketi yaliyorushwa na askari wa Ethiopia wakati ndege ya shirika la Africa Express Airways ilikuwa inajaribu kutua, lakini hadi katika hatua hii hakuna kinachothibitisha madai hayo.

Jumatano wiki hii Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia pia ilielezea kuguswa na tukio hilo. Jambo ambalo ni nadra sana kwa Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.