Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-USALAMA

Wawili wauawa katika makabiliano kati ya wafuasi wa Uhuru Kenyatta William Ruto

Watu wawili wameuwa na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa makabiliano kati ya wafuasi wa rais wa Kenya Uhuru na Kenyatta na naibu wake William Ruto katika Kaunti ya Muranga, nchini Kenya.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia) na Makamu wa tais William Ruto.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia) na Makamu wa tais William Ruto. Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vurugu zilizuka baada ya wafuasi wa rais Kenyatta kudaiwa kujaribu kumzuia Ruto kuhudhuria kuhudhuria ibada katika ngome ya rais Kenyatta na kuwalazimu polisi kuingilia kati na kuwarushia mabomu ya machozi kuwasambaratisha.

Uhusiano wa rais Kenyatta na naibu wake unaonekana kuwa baridi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022, baada ya kile ambacho wachambuzi wa siasa wanaema ni hatua ya Ruto kuanza kampeni za mapema kinyume na maelekezo ya rais wa nchi hiyo.

Uhuru Kenyatta na Wiliam Ruto waliingia madarakani wakiahidi kuunganisha taifa na kukomesha migawanyiko ya kisiasa, lakini serikali yao imelaumiwa kwa kuzidisha migawanyiko ya kikabila na ufisadi ambao umesababisha nchi kupoteza mamilioni ya dola - ikiwemo dola milioni 7.8 za kununua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa hatari wa Covid 19, ambayo sasa inaasadikiwa huenda zimeibiwa.

Ruto anapania kumrithi Kenyatta kama rais mwaka 2022 lakini anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wafuasi wa Kenyatta wanaodai kuwa ameanza kufanya kampeni mapema miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.