Pata taarifa kuu
UGANDA-CORONA-AFYA

Wanafunzi na walimu kupimwa virusi vya Corona kabla ya kufunguliwa kwa shule Uganda

Wizara ya afya nchini Uganda inasema Wanafunzi na Walimu wanaoishi katika maeneo yenye maambukizi makubwa ya virusi vya Corona, watapimwa iwapo wana maambukizi kuelekea kufunguliwa kwa Shule na taasisi zingine za elimu ya Juu nchini humo.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Uganda, Kampala. REUTERS/James Akena/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi wa mwaka wa mwisho waliotarajiwa kufanya mtihani kabla ya kuzuka kwa janga la Corona ndio watakaoruhusiwa kuanza kurejea Shuleni.

Mwishoni mwa wiki iliyopita rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza kuwa shule na taaissi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwezi ujao. Hatua hiyo inakuja wakati Uganda kufikia sasa imerekodi visa zaidi ya 6,287 vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Museveni alisema wanafunzi hao watarejea shuleni kuanzia tarehe 15 Oktoba, na mikakati imewekwa kuhakikisha kuwa wanakuwa salama.

Shule zilifungwa nchini humo mwezi Machi baada ya kuzuka kwa janga hilo ambalo limewaambukiza watu zaidi 6,287 na wengiene zaidi ya 63 kupoteza maisha.

Virusi vya Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).

Virusi vipya vya Corona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya Corona ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.