Pata taarifa kuu
KENYA-UAE-HAKI-CORONA

Wakenya zaidi ya 400 waliokwama Dubai waomba kurejeshwa nyumbani

Mamia ya raia wa Kenya ambao walikwenda katika nchi ya Falme za Kiarabu wamekwama mjini Dubai baada ya kushindwa kurudi nyumbani baada ya safari za ndege kusitishwa na kupoteza ajira kutokana na janga la Corona.

Raia wa Kenya ni miongoni mwa Waafrika wengine waliokwama nje ya nchi zao baada ya kufungwa kwa safari za ndege kutokana na janga la Corona na ahueni yao ni kurejea nyumbani.
Raia wa Kenya ni miongoni mwa Waafrika wengine waliokwama nje ya nchi zao baada ya kufungwa kwa safari za ndege kutokana na janga la Corona na ahueni yao ni kurejea nyumbani. dubaiairshow.aero
Matangazo ya kibiashara

Wakenya hao ni miongoni mwa waafrika wengi ambao wanatamani kurudi nyumbani.

Wengi hawana mahali pa kuishi, hawana chakula na wamesalia ombaomba katika nchi walioyokwenda kutafuta kazi.

Ombi lao ni moja tu, wanataka kurudi nyumbani.

Wanadai juhudi za kupata usaidizi kupitia Ubalozi wa nchi yao hazijafua dafu.

Serikali ya Kenya kuptia msemaji wake, Cyrus Oguna, inasema inafamu changamoto za raia wake waliokwama huko Dubai.

Raia hawa wa Kenya ni miongoni mwa Waafrika wengine waliokwama nje ya nchi zao baada ya kufungwa kwa safari za ndege kutokana na janga la Corona na ahueni yao ni kurejea nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.