Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-USALAMA

Jeshi la Sudan Kusini latangaza kifo cha kiongozi wa waasi Kerbino Wol

Askari huyu wa zamani aliyebahatikiwa kuwa mjasiriamali baada ya kurejeshwa katika maisha ya kiraia alifungwa kwa muda wa miezi ishirini nchini Sudani Kusini.

Vikosi vya Ulinzi vya Sudan Kusini, lililokuwa likijulikana kama Jeshi la Ukombozi la watu wa Sudan, wakati wa mazoezi karibu na Juba, Aprili 26, 2019.
Vikosi vya Ulinzi vya Sudan Kusini, lililokuwa likijulikana kama Jeshi la Ukombozi la watu wa Sudan, wakati wa mazoezi karibu na Juba, Aprili 26, 2019. REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Alipofunguliwa mwezi Januari, Kerbino Wol aliamua kuanzisha kundi la waasi, aliloliita Oktoba 7, mwanzoni mwa mwezi huu.

Hata hivyo vikosi vya usalama vimetangaza kwamba vilimwua katikati mwa nchi siku ya Jumapili baada ya siku nne za mapigano.

Kerbino Wol ameuawa siku kumi tu baada ya kuanzisha kundi lake la waasi. Ameuawa na wapiganaji wake kwa kupigwa risasi katika kijiji kimoja "wakati walikuwa wanakwenda kutekeleza shambulio dhidi ya jeshi na hakutaka kufanya mazungumzo," amesema msemaji wa vikosi vya ulinzi. Meja Jenerali Lul Ruai Koang ameongeza kuwa ujasusi ndio uliwawezesha kumpata kiongozi huyo na kumuangamiza yeye na wapiganaji wake.

Kerbino Wol, yeye na familia yake walikimbilia Ethiopia wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Khartoum, wakati Sudan ilikuwa bado nchi moja. alipokuwa uhamishoni, alisajiliwa katika jeshi Nyekundu, kitengo cha askari wa watoto. Tangu wakati huo alishiriki mapigano upande wa waasi, alitumika kama mlinzi au hata alifanya kazi kwa idara ya ujasusi.

Baada ya vita, alirejeshwa katika maisha ya kiraia na kuwa mjasiriamali. Baada ya kupokea dola 200, kama posho kwa waasi wanaorejeshwa katika maisha ya kiraia, alianzisha kampuni iitwayo KASS, ambayo sasa ni moja ya kampuni binafsi zinazoongoza za ulinzi nchini, ikiajiri vijana 2000.

Kerbino Wol alikamatwa mnamo mwezi Aprili 2018na idara ya ujasusi na kuzuiliwa kwa muda wa miezi kadhaa bila kufunguliwa mashitaka. Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International mara nyingi lilishutumu kifungo chake.

Mwishowe alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano kwa kosa la kuanzisha uasi, na aliachiliwa huru mnamo mwezi Januari kwa msamaha wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.