Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-USALAMA

Watu 400 wauawa katika machafuko ya kikabila Sudan Kusini

Zaidi ya watu 400 wameuawa katika muda wa wiki mbili zilizopita nchini Sudan Kusini kutokana na mapigano ya kijamii kwenye majimbo matano nchini humo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwa na Riek Machar (kulia) Februari 20, 2020 huko Juba.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwa na Riek Machar (kulia) Februari 20, 2020 huko Juba. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Wakati zaidi ya wananchi milioni kumi na moja wa Sudan Kusini wanapambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, kumezuka vuruga ya kijamii ambayo imesababisha vifo vya zaidi ya watu mia nne katika majimbo matano kati ya majimbo kumi ya nchi hiyo: Jonglei, Warrap, Central Equatoria, Lakes na Western Bahr El Ghazal.

David Shearer, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, amethibitisha mauaji hayo katika majimbo hayo matano.

“Mamia ya watu wameuawa. Licha ya ugonjwa wa Covid-19, vikosi vya Umoja wa mataifa vinahakikisha kuwa vurugu zimekoma. Kukosekana kwa usalama nchini Sudani Kusini kunasababishwa na kucheleweshwa kuteuliwa kwa magavana katika majimbo. Zoezi hilo linatakiwa litekelezwe haraka iwezekanavyo ili amani irejee, “ David Shearer amesema.

Uingereza, Norway na Marikani, zilichangia pakubwa katika kuhakikisha kuwa kuna serikali mpya nchini Sudan Kusini.

Msemaji maalum wa nchi hizo, Jonathan Sibra, amemtolea wito rais Salva Kiir na washirika wake serikalini kuhakikisha usalama na amani vimepatikana haraka iwezekanavyo.

“Huu ndio wakati mwafaka ambao rais na makamu wake wote sita wanaweza kukubaliana kuhusu uteuzi wa magavana na kuendelea kutawala pamoja kwa minajili ya raia wa Sudan Kusini. Kucheleweshwa zaidi kwa uteuzi huo kutasababisha machafuko zaidi, “ amesema Jonathan Sibra.

Sudani Kusini imeendelea kukumbwa na visa mbalimbali vya mauaji na mdororo wa usalama, huku raia wengi wakiyatoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.