Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAZINGIRA-AFYA

Mvua kubwa yaongeza kitisho kwa machafuko yanayoendelea Sudani Kusini

Sudani Kusini inaenelea kukumbwa na mvua kubwa tangu mwezi Julai mwaka huu na sasa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni moja wameathiriwa na mvua hiyo.

Mafuriko katika eneo la Panthau, Sudani Kusini, mwaka 2017.
Mafuriko katika eneo la Panthau, Sudani Kusini, mwaka 2017. © Albert Gonzalez Farran / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kanda za kaskazini na mashariki zinaendelea kuathiriwa. Hali ya kipekee ambayo inadhoofisha nchi hii katika hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari inakabiliana nayo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hali hii haijawahi kutokea katika miongo kadhaa iliyopita. Kulingana na utabiri bado mvua hii itaendelea kunyesha kwa wiki kadhaa, wakati msimu wa kiangazi ungelikuwa tayari umeanza.

Mashirika ya kihisani yameanza kutuma timu zao na uwezo wao kwa kukabiliana na hali hiyo. "Ni janga," amesema Sajit Menon.

"Watu hawa wamekuwa wakikabiliana na njaa. Walmekimbilia kwenye milima. Tunapaswa kuwakuta huko kabla hali haijawa mbaya kabisa. Maisha yao yako hatarini, "mwakilishi wa shirika la kihisani la Oxfam nchini Sudani Kusini Sajit Menon amesema.

Changamoto ni kubwa katika nchi hii iliyo na kilomita 200 tu za barabara zilizo na lami.

Hali hiyo inasababishwa zaidi na uharibifu wa miundombinu muhimu kama vituo vya afya. Katika mji wa Pibor, shirika la Madaktari wasio na Mipaka, MSF limejikuta hospitali yake imejaa maji kutokana na mafuriko. Wagonjwa wamelazimika kurejeshwa nyumbani.

Mvua hiyo imeharibu heka 17,000 za mashamba, tani 20,000 za chakula, maelfu ya mifugo. Wakati 60% ya raia tayari wako katika hali ya kukabiliwa na ugonjwa wa utapiamlo, takwimu hiyo inaweza kuongezeka zaidi.

Pamoja na mafuriko, watu wana hofu ya kutokea milipuko ya ugonjwa wa Malaria, hepatitis A na magonjwa ya kuhara. Ugonjwa wa Kipindupindu, ingawa ulitoweka tangu mwaka mmoja uliyopita, unaweza kurudi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.