Pata taarifa kuu
KENYA-MALARIA-CHANJO-AFRIKA

Chanjo ya Malaria yaanza kutolewa nchini Kenya

Kenya linakuwa taifa la tatu barani Afrika kuanza kutumia chanjo ya ugonjwa wa Malaria baada ya Ghana na Malawi.

Mbu anayesambaza Malaria
Mbu anayesambaza Malaria AFP/PHILIPPE HUGUEN
Matangazo ya kibiashara

Chanjo hiyo inaanza kutolewa siku ya Ijumaa, ambapo watoto 300,000 wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo kila mwaka.

Hatua hii inakuja, baada ya chanjo hiyo inayofahamika kama RTS kuwa katika matengenezo kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Watalam wa afya wanasema kuwa chanjo hiyo itasaidia kuwauwa wadudu wa Malaria ambao husambaa mwilini baada ya mtu kunga'twa na mbu anayesambaza ugonjwa huo.

Tayari WHO inasema kuwa, majaribio ya chanjo hii yameonesha kuwa inafanya kazi, baada ya kubainika kuwa watoto wane kati ya kumi waliopewa chanjo hiyo walipata kinga dhidi ya Malaria.

Malaria unasalia ugonjwa hatari hasa kwa watoto barani Afrika na huwauwa watoto zaidi ya 400,000 kila mwaka duniani, wengi wakiwa barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.