Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-HAKI

Burundi yakosoa msimamo wa Umoja wa Afrika kufuatia waranti wa kumakamata Buyoya

Serikali ya Burundi imeshtumu Umoja wa Afrika kwa msimamo wake kufuatia waranti wa kumkamata rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya, baada ya kumshtumu kwamba alihusika kwa mauaji ya aliyekuwa rais wa kwanza kutoka Kabila la Wahutu Melchior Ndadaye, aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka 1993.

Pierre Buyoya, rais wa zamani wa Burundi na Mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Afrika nchini Mali na katika eneo la Sahel.
Pierre Buyoya, rais wa zamani wa Burundi na Mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Afrika nchini Mali na katika eneo la Sahel. RFI
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika umeionya Burundi dhidi ya hatua zinazoweza kuhujumu mchakato wa amani baada ya kutolewa waranti wa kimataifa wa kumkamata rais wa zamani Pierre Buyoya na maafisa wengine 16.

Hivi karibuni Bw Buyoya alipinga vikali madai kuwa alihusika kwenye kifo cha Bw Ndadaye.

Buyoya amesema katika taarifa kuwa "Kila kitu kinaonesha kuwa huo ni mpango wa kisiasa unaolenga kumchafua na ni mwelekeo mpya wenye lengo la kusahaulisha maumivu ya masuala ambayo bado hayajapatiwa suluhu tangu kuanza kwa mgogoro wa kisiasa nchini humo mwaka 2015.

Tayari maafisa kadhaa wa zamani wa jeshi la Burundi (Ex FAB) wamekamatwa na wengine wanaendelea kutafutwa, huku mali zao nchini zikizuliwa.

Kuuliwa kwa Melchior Ndadaye kulisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Zaidi ya watu 300,000 waliuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi lenye watutsi walio wachache na waasi wa Kihutu vilivyodumu miaka 12. Wakati huo maelfu ya watu walilazimika kutoroka makazi yao na kukimbili nchi jirani.

Kuna hofu kuwa kumlenga Bw Buyoya ambaye ni kutoka kabila la Watutsi anayeishi nchini Mali kunaweza kuchangia kuzuka misukosuko ya kikabila.

Bw Buyoya ambaye alitwaa madaraka mara mbili ndani ya miongo mitatu iliyopita kwa msaada wa jeshi ni mwanadiplomasia anayeheshimiwa barani Afrika.

Buyoya 69, alihusika kwenye mchakato wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongoza kuchaguliwa kiongozi wa zamani wa waasi wa Hutu Pierre Nkurunziza kuwa rais mwaka 2005.

Wadadisi wanasema hatua ya utawala wa Nkurunziza kutoa waranti wa kimataifa wa kumkamata Pierre Buyoya inalenga kupotosha jumuiya ya kimataifa kwa hali inayojiri nchini humo, ikiwa ni pamoja na kukataa kushiiki mazungumo, ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.