Pata taarifa kuu
BURUNDI-RWASA-SIASA

Agathon Rwasa aendelea kutengwa katika siasa nchini Burundi

Mamlaka nchini Burundi zimekataa kusajili chama kipya cha National Liberty Front kilichoanzishwa hivi karibuni na kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Agathon Rwasa.

Agathon Rwasa, mmoja kati ya wanasiasa wakuu wa upinzani Burundi.
Agathon Rwasa, mmoja kati ya wanasiasa wakuu wa upinzani Burundi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Rwasa alianzisha chama cha National Liberty Front au Amizero y'Abarundi baada ya kupitishwa kwa mabadiliko ya katiba mwezi May mabadiliko ambayo yanakataza muungano wa wagombea binfasi kushiriki kwenye uchaguzi.

Licha ya mara kadhaa Rwasa kuonekana kutokuwa mpinzani wa kweli kwa chama tawala cha CNDD-FDD, muungano wake wa Amizero y'Abarundi ulipata asilimia 17 ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Hivi karibuni Agathon Rwasa, mwanasiasa mkongwe na mashuhuri wa upinzani nchini Burundi, alisema itawalazimu wanasiasa wa upinzani kujidhatiti katika vyama vyao ili baadae kujiweka pamoja wakati wa mpambano wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba mpya.

Kwa sasa Rwasa ni Makamu Spika wa Bunge na alikuwa akiwakilisha mseto wa vyama vya upinzani wa Amizero y'Abarundi.

Muungano huo katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ulishika nafasi ya pili ukitanguliwa na chama tawala CNDD FDD cha Rais Pierre Mkurunziza.

Rwasa amewahi kuishi uhamishoni katika nchi jirani ya Tanzania kwa takribani miaka 20 alipotoroka uongozi wa watutsi wachache.

Agathon Rwasa alitoroka tena mchi mwaka 2010 wakati CNDD FDD ikiongoza. Baadae alirejea Burundi 2013.

Agathon Rwasa aliporejea mjini Bujumbura akitokea mafichoni, Agosti 6, 2013.
Agathon Rwasa aliporejea mjini Bujumbura akitokea mafichoni, Agosti 6, 2013. AFP PHOTO/Esdras Ndikumana

Alijiunga na bunge baada ya uchaguzi wa 2015 ulio susiwa na upinzani

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.