Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Upinzani watoa mapendekezo kuhusu kurejea kwa amani Burundi

Wakati mkutano wa wanasiasa wa ndani na wale wanaoishi nje kutoka Burundi katika mazunguzo ya kusaka suluhusu ya amani mjini Arusha nchini Tanzania ukielekea kumalizika, wanasiasa hao wamebaini wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa kuzuka vita kutokana na hatua ya serikali ya Bujumbura kususia mazungumzo.

Agathon Rwasa, mmoja kati ya wanasiasa wakuu wa upinzani Burundi.
Agathon Rwasa, mmoja kati ya wanasiasa wakuu wa upinzani Burundi. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Baada ya vikao vya siku tano, wajumbe katika kile kinachodaiwa kuwa mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi wametoa mitazamo yao kuhusu kile kinachoweza kufanyika ili kuzua uwezekano wa kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi.

Hii imekuja baada ya muwezeshaji katika mazungumzo hayo rais wa mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa kukiri kwamba juhudi zake za kuwaleta pamoja wadau wote katika mzozo wa Burundi zimekwamishwa na serikali ya Burundi.

Ilitarajiwa kuwa kikao kilichoanza Octoba 24 kingelikuwa cha mwisho katika mlolongo wa vikao vya kuwakutanisha washikadau wote katika mzozo wa Burundi ulioanza tangu mwaka 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Taarifa kutoka Arusha zinaeleza kuwa wajumbe waliopo katika vikao vinavyofanyika faraghani wametia saini jana usiku katika mapendekezo yao kuhusu namna mzozo wa Burundi unavyoweza kupatiwa suluhusu, mpango ambao uantarajiwa kuwasilishwa leo Jumatatu kwa muwezeshaji Benjamin Mkapa na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.