Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-HAKI-USALAMA

Chama cha Ingabire chastumu rais wa Rwanda kwa kauli yake

Baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame kutowa tahadhari kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire ambae alisikika kwenye vyombo vya habari kwamba aliachiwa huru kutokana na shinikizo na sio kwa msamaha wa rais, chama chake kimebaini maskitiko kutokana na kauli ya rais Kagame.

Victoire Umuhoza Ingabire, kiongozi wa chama cha upinzani Rwanda cha FDU.
Victoire Umuhoza Ingabire, kiongozi wa chama cha upinzani Rwanda cha FDU. home.planet.nl
Matangazo ya kibiashara

Paul Kagame aliwakemea wale wote wanaosema kwamba hatuwa ya kuachiwa huru kwa wafungwa akiwemo mwanasiasa Ingabire na Kizito Mihigo ilitokana na shinikizo kutoka katika mataifa ya magharibi, jambo ambalo alisema hakuna anaeweza kuwashinikiza wanyarwanda kwa lolote.

Joseph Bukeye Kada wa chama cha Victoire Ingabire, FDU, amesema kauli ya rais Kagame ni dhahiri kwamba anachanganya Mamlaka yake na mamlaka za vyombo vya sheria maana swala la nani aitwe mbaroni ni la Mahakama na sio rais anaeamuwa.

β€œKatika demokrasia, kwenye nchi yenye kuheshimu sheria, sivyo ambavyo swala linatakiwa kuamuliwa, kama bi Ingabire amekwenda kinyume na sheria, ni swala la vyombo vya sheria kuamuwa kumpeleka jela au la, na sio rais anaeamuwa nani anakwenda jela na nani haendi jela. Hili linaonyesha wazi ukosefu wa kutofautisha madaraka. Nchi ambayo inawania uongozi wa taasisi ya nchi zinazozungumza Kifaransa iliotia kipao mbele katika uheshimishwaji wa haki za binadamu, ni ajabu sana kuona nchi hiyo hiyo inapuuzia swala la haki za binadamu. Inaonyesha wazi kwamba bado tuko mbali katika swala la haki za binadamu”, ameshtumu Joseph Bukeye.

Akihotubia bunge baada ya wabunge waliochaguliwa hivi karibuni kuapishwa rasmi, rais Kagame amesema msamaha aliotoa β€œndiyo njia” aliyochagua ya kutatua matatizo na kujenga taifa hla Rwanda.

Victoire Ingabire alipotoka gerezani alimshukuru rais Kagame kwa msamaha wake lakini akasisitiza kuwa hakuomba msamaha kwa kuwa hakufanya kosa lolote.

Bi Ingabire , ambaye ni kutoka kabila la wahutu, alikamatwa na kufungwa baada ya kuhoji ni kwa nini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda ya 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Wahutu. Alishtumiwa kuchochea chuki na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, kabila la rais Paul Kagame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.