Pata taarifa kuu
RWANDA-AU

Kesi ya Ingabire dhidi ya serikali ya Rwanda kuanza katika Mahakama ya Afrika

Mahakama ya Afrika inayoshughulikia maswala ya haki za binadamu yenye makao yake mjini Arusha nchini Tanzania, inaanza kusikiliza kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Victoire Umuhoza Ingabire, anayedai kuwa serikali ya Rwanda imedhulumu haki zake za kisiasa na haki za binadamu.

Victoire Ingabire (Kulia) akiwa na Wakili wake  Ian Edwards, Mahakamani mwaka 2011
Victoire Ingabire (Kulia) akiwa na Wakili wake Ian Edwards, Mahakamani mwaka 2011 AFP PHOTO/Steve Terrill
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii inafanyika licha ya tishio la serikali ya Rwanda kuwa inataka kujiondoa katika Mahakama hiyo ya Afrika.

Bi, Ingabire ambaye alihukumiwa jela kwa miaka 15 anadai kuwa haki zake zilidhulumiwa wakati kesi yake ilipokuwa inaendelea hali anayosema iliendelea hadi kuhukumiwa kwake.

Kiongozi huyo wa chama cha FDU-Inkingi, anataka Mahakama hiyo ya Afrika kuamuru kuachiliwa kwake mara moja na kuipata serikali ya Rwanda na kosa la kudhulumu haki zake.

Kupitia Mawakili wake, Ingabire pia anataka Mahakama hiyo kuamua kuwa kesi dhidi yake haikufanyika kwa haki.

Mwanasiasa huyo na mpinzani wa rais Paul Kagame, alishtakiwa na kufungwa jela kutokana na matamshi yake ya kupinga kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, yaliyosababisha zaidi ya watu 800,000 kupoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.