Pata taarifa kuu
RWANDA

Kiongozi wa Upinzani Nchini Rwanda Ingabire kukata rufaa akipinga adhabu ya kifungo cha miaka 8 jela

Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire Umuhoza ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela kutokana na kukutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini lakini tayari Wakili wake Ian Edwards amesema watakata rufaa kupinga adhabu aliyopewa mteja wake.

Kiongozi wa Upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire Umuhoza akiwa na Wakili wake Ian Edwards mahakamani
Kiongozi wa Upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire Umuhoza akiwa na Wakili wake Ian Edwards mahakamani AFP PHOTO/Steve Terrill
Matangazo ya kibiashara

Mawakili wanaomtetea Ingabire wakiongozwa na Edwards wamesikitishwa na hukumu hiyo wakidai haikustahili kutolewa dhidi ya mteja wao kutokana na Kiongozi huyo wa Upinzani kutoshiriki kwa namna yoyote kwenye mashtaka ambayo yalifunguliwa dhidi yake.

Ingabire mwenye ambaye hakuhudhuria Mahakamani na badala yake akasalia jela alikowekwa tangu mwezi Oktoba mwaka 2010 ameendelea kusisitiza kutotenda makosa ambayo yameelekezwa kwake akidai kile kinachofanyika kinamsukumo wa kisiasa na hivyo haki haijatendekea.

Wakili Edwards kwa upande wake amesema wataanza kukata rufaa katika Mahakama Kuu na iwapo watashindwa rufaa yao wataelekea katika Mahakama ya Afrika inayoshughulikia Haki za Binadamu ili kuhakikisha mteja wao anapata haki yake.

Naye Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Barani Afrika Daniel Bekele amekiri Ingabire kutopata hukumu yenye haki huku akieleza sababu ambazo zinawafanya waamini hivyo ni pamoja na uwepo wa msukumo wa kisiasa, uhalali wa ushahidi ambao umetumika pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali kueleza hukumu kabla ya Mahakama kutoa maamuzi.

Jaji ambaye alikuwa anasikili kesi ya Ingabire, Alice Rulisa aliiambia mahakama wamemkuta na hatia ya kutenda makosa ya uhaini kutokana na kufadhili vikundi vya kigaidi pamoja na kukataa ushiriki wake kwenye mauaji ya kimbari yaliyofanyika nchini humo mwaka 1994.

Rulisa ameweka bayana wamemkuta na hatia Ingabire ya kushiriki kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu laki nane nchini humo huku wengi wao wakiwa ni Watutsi.

Ingabire ambaye ni Mhutu na Kiongozi wa Chama Cha FDU alirejea nchini Rwanda mwaka 2010 mnamo mwezi Januari baada ya kuishi uhamishoni nchini Uholanzi baada ya kutajwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.