Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA-MAREKANI-AL QAEDA-USALAMA

Shambulizi dhidi ya ubalozi Marekani: Kenya na Tanzania waadhimisha kumbukumbu ya miaka 20

Kenya na Tanzania zinaadhimisha miaka 20 tangu kutokea kwa shambulizi la bomu katika ubalozi wa Marekani jijini Nairobi na Dar es salaam mwaka 1998. Baadhi ya waliofikwa na kadhia hiyo bado hawajafidiwa

Mji mkuu wa Kenya ambako  shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani lilitokea mnamo mwaka 1998.
Mji mkuu wa Kenya ambako shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani lilitokea mnamo mwaka 1998. Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Agosti 7 ni kumbukumbu ya miaka 20 tangu kutokea milipuko pacha ya mabomu katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998 na kusababisha mamia kufariki.

Aprili, 2014 jaji katika mahakama ya Washington DC aliotoa uamuzi kwamba Watanzania na Wamarekani 23 waliokufa au kujeruhiwa katika shambulizi la ubalozi jijini Dar es Salaam walipaswa kulipwa fidia ya Dola za Marekani 957 milioni.

Hali ilikuwa mbaya sana nchini Kenya, baada ya shambulizi hilo kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na zaidi ya 5000 kujeruhiwa.

Nchini Kenya, raia zaidi ya 200 wa nchi hiyo walipoteza maisha huku Wamarekani 12 nao wakiangamia.

Mwaka huohuo mahakama ya New York, iliwapa haki ya kulipwa Dola 1 bilioni raia wengine sita wa Kenya walioathirika na shambulizi la bomu jijini Nairobi.

Hata hivyo, iliamuliwa kuwa fidia itapatikana baada ya kukamatwa na kutaifishwa mali kutoka kwa kundi la Al- Qaeda lililotuhumiwa kuhusika na mashambulizi hayo.

Waathirika wa milipuko hiyo 538 raia wa Kenya wanasema hata kama itawachukua miaka 30 kupata haki yao, hawatakata tamaa kupigania wanachoamini ni haki yao.

Mwanasheria anayewawakilisha watu hao, Philip Musolini alinukuliwa Jumapili na gazeti la Sunday Nation la Kenya akisema wameanza kuwasiliana na baadhi ya wabunge wa Bunge la Congress kushawishi kufanyika marekebisho ya sheria ya fidia iliyopitishwa mwaka 2015 inayotoa fidia kwa raia wa Marekani walioathirika kwenye mashambulizi.

Alisema licha ya Congress kutoonyesha ishara yoyote kwamba marekebisho yatafanyika hivi karibuni, lakini ana matumaini njia hiyo itazaa matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.