Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-USHIRIKIANO-DIJITALI

Rais wa Rwanda Paul Kagame azuru Ufaransa

Rais wa Rwanda Paul Kagame anafanya ziara ya siku mbili nchini Ufaransa. Rais wa Rwanda atashiriki siku ya Alhamisi wiki hii katika maonyesho ya Viva Technologies, maonyesho ya kimataifa kuhusu masuala ya kidijitali.

Rais wa Rwanda Paul Kagame katika Mkutano wa kimataifa wa Afya Geneva Mei 21, 2018.
Rais wa Rwanda Paul Kagame katika Mkutano wa kimataifa wa Afya Geneva Mei 21, 2018. Fabrice COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya hapo, atakaribishwa Jumatano wiki hii katika Ikulu ya Elysee, kwanza kwa chakula cha mchana na wadau wa mkutano huo, kisha kwa mazungumzo na mwenyeji wake Emmanuel Macron. Emmanuel Macron na Paul Kagame watafanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. Ishara kwamba joto linaendelea kuongezeka kati ya Paris na Kigali, wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizi mbili ulikua si mzuri tangu miaka ya 1994.

Ziara ya rais Paul Kagame nchini Ufaransa inakuja ikiwa ni miaka mitatu toka azuru nchi hiyo ya Ulaya ambayo Rwanda imekua ikiishtmu kusaidia chama cha MRND cha hayati rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana na wanamgambo wa kihutu wa Interahamwe wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Maonyesho ya Viva Technologies kwa mwaka huu yameelekezwa Afrika, na ujio wa Rais wa Rwanda ulikuwa unatarajiwa kabisa, chanzo kutoka Elysee kimebaini. Paul Kagame ni mmoja wa viongozi wa uvumbuzi katika bara la Afrika, chanzo kimeongeza.

Katika muktadha huu, Rais Kagame atakula chakula cha mchana na wadau kadhaa wanaoongoza katika masuala ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na Mark Zuckerberg, Mkuu wa mtandao wa Facebook, kabla ya kutembea kesho na Emmanuel Macron katikamaonyesho hayo kuhusu dijitali.

Lakini sio maswali tu ya uvumbuzi ambayo yalimfanya Paul Kagame kuzuru Ufaransa. Rais Paul Kagame amefanya safari ya kukutana na mwenzake wa Ufaransa leo mchana. Mazungumzo kati ya wawili hawa yatafanyika katika ikulu ya Elysee ambako rais wa Rwanda hajafika tangu mwezi Septemba 2011.

Umoja wa Afrika kwenye ajenda ya mazungumzo

Emmanuel Macron na Paul Kagame wanatarajia kuzungumzia juu ya Umoja wa Afrika ambapo Paul Kagame ni rais wa taasisi hiyo tangu mwezi Januari mwaka huu. Kwa hiyo, rais Kagame amekuja na masuala mawili ya mageuzi kuhusu ufadhili wa shughuli za kulinda amani na kuhusu Umoja wa Afrika.

Suala jingine ambalo litajadiliwa na wawili hao ni kuwania kwa Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, kwenye nafasi ya mkuu wa Jumuiya ya Nchi zinazozungumza Lugha ya Kifaransa "Francophonie" (OIF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.