Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-DIPLOMASIA

Rwanda yasema uhusiano wake na Ufaransa unaanza kuimarika

Serikali ya Rwanda inasema imeanza kuridhishwa na uhusiano mwema kati yake na Ufaransa, ikisema hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa na rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron zinatia moyo.

Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda
Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda AFP PHOTO/ TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuingia madarakani kwa rais Macron, amekutana mara kadhaa na rais wa Rwanda Paul Kagame na kufanya naYe mazungumzo ambayo sasa waziri wa mambo ya nje wa Rwanda ambaye pia ni Waziri wa habari nchini humo Louse Mushikiwabo, anasema yamekuwa na tija.

Kwa miongo kadhaa Rwanda imekuwa haina uhusiano mzuri na Ufaransa tangu nchi hiyo ituhumu Ufaransa kwa kuhusika kwenye kuchochea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

"Tangu  kuingia madarakani kwa serikali mpya, rais Macron ameonesha nia ya kuimarisha uhusiano huu. Huenda ukachukua muda mrefu lakini nina imani mambo hakiendelea hivi yatakwenda vema, siis Rwanda tuko tayari," alisema.

Kwa upande mwingine Mushikiwabo pia ameeleza kuhusu kutokuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya nchi yake na Uganda lakini akasema anatumaini kuwa tofauti zilizojitokeza zitatatuliwa hivi karibuni ili kurejea kwa uhusiano wa kawaida.

Aidha, wakuu wa nchi 26 wa nchi za Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Kigali kuanzia juma lijalo kwaajili ya kutia saini mkataba wa eneo la biashara huru wa bara la Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.