Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-USALAMA

Makamu wa rais wa Sudan Kusini ashtumu viongozi wa dini kushochea vurugu

Makamu wa rais wa Sudan Kusini James Wani Igga amewashtumu viongozi wa dini nchini humo kwa kuhubiri chuki dhidi ya serikali na kuchochea machafuko.

Makamu wa Rais wa Sudan Kusini James Wani Igga (katikati), akiongozana na Rais Salva Kiir (kulia) na aliyekua Makamu wa rais Machar (kushoto), katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu Juba, Julai 8, 2016.
Makamu wa Rais wa Sudan Kusini James Wani Igga (katikati), akiongozana na Rais Salva Kiir (kulia) na aliyekua Makamu wa rais Machar (kushoto), katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu Juba, Julai 8, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Igga amesema viongozi hao wamekuwa wakiwaambia raia wa taifa hilo kuwa, rais Kiir ni kiongozi mbaya matamashi ambayo amesema ni ya uchochezi.

Viongozi wa Makanisa nchini Sudan Kusini wamekuwa wakimshutumu rais Kiir kwa kuendeleza vita nchini humo na kukataa kuheshimu mikataba ya amani kati yake na makundi ya waasi.

Hivi karibuni Global Witness, Shirika la Kimataifa linalochunguza mizozo, matumizi mabaya ya rasilimali na ufisadi, ilitoa ripoti inayooonesha namna viongozi wa Sudan Kusini wanavyotumia Mamilioni ya Dola kufadhili vita vinavyoendelea nchini humo.

Uchunguzi wa Global Witness umebaini kuwa fedha zinazopatikana kutoka kwenye kampuni ya Nile Petroleum au Nilepet, zinatumiwa kukunua silaha zinazotumiwa kupambana na wapinzani wa serikali ya Juba.

Kampuni hiyo inafanya kazi zake kwa siri na mbali na rais Kiir, watu wengine wanaonufaika ni washauri wake wa karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.